Tuesday, June 12, 2012


Hana, 12, amwonyesha dadake Eva, kidole cha ushindi, huku wakiendelea kupata matibabu baada ya nyumba yao kushambuliwa
Afisa mkuu anayehusika na masuala ya watoto na mizozo, Radhika Coomaraswamy, ameiambia BBC kuwa hajawahi kushuhudia hali kama hiyo ambapo watoto hawahurumiwi na kulengwa kwenye mashambulio.

Akizungumza kutoka makao makuu ya Umoja wa Mataifa, Coomeraswamy ameiambia BBC kuwa ni jambo la kawaida kuwaona watoto wakiuawa au kujeruhiwa wakati wa vita, lakini ameongezea kuwa ni jambo la kusikitisha kuona watoto wanateswa na kudhulumiwa wakiwa kizuizini au hata kuuawa kinyama, kama vile wanavyotendewa nchihi Syria na wanajeshi wa serikali.

Pia amewashutumu wapiganaji wa upinzani wa Free Syrian Army kwa kuwatumia watoto chini ya umri wa miaka kumi na sita katika mstari wa mbele wa mapigano.
Coomeraswamy amesema watoto kadha wamejitokeza na kudai kuwa walitekwa nyara na kulazimishwa kuabiri magari ya kivita na kutumiwa kama ngao na wanajeshi wa nchi hiyo.

Ameongeza kuwa makundi kadhaa ya waasi pia yamewasajili watoto walio na umri wa chini ya miaka kumi na sita kuwa wanajeshi wao. Wengi wao wanatumiwa kama wahudumu wa afya na pia kama mabawabu mbali na kuwekwa katika mstari wa mbele wa vita.
Bi Coomeraswamy sasa amejumuisha wanajeshi wa Syria katika orodha ya Umoja wa Mataifa ya mataifa yanayowadhulumu na kuwauawa watoto, kushambulia shule na hospitali mbali na kuhusika na visa vingine vya ukiukwaji wa haki za kibinadamu.

Mataifa mengine ambayo yamewekwa kwenye orodha hiyo afghanistan na Iraq pia yamejumuishwa kwenye orodha hiyo ya aibu.
Amesema mzozo wa kisiasa nchini syria umepoteza mwelekeo na kuwa wanajeshi wa serikali na waasi hawatofautishi raia na maadui wao na hivyo wanachukua maamuzi ya pamoja ambayo watoto wanalengwa

0 comments:

Post a Comment