Saturday, June 16, 2012

KLABU ya Simba imefuta mpango wa kumsajili nyota wake wa zamani, Dany Mrwanda, anayechezea klabu ya DT Long An ya Vietnam, imefahamika.
Simba pia imeachana na mpango wa kumsajili beki, Shadrack Nsajigwa, aliyetemwa na Yanga hivi karibuni kutokana na kushuka kiwango.

Chanzo cha uhakika kutoka ndani ya Simba, kimesema, wameachana na Mrwanda kutokana na masharti magumu.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, kati ya masharti hayo, ni kutaka apewe shilingi mil.12 kama wanataka asaini mktaba.

“Tumeamua kuachana na Mrwanda, masharti yake mengi, mbali ya kutaka sh mil.12, pia anataka tuwe tayari kumruhusu kwenda nje akitakiwa,” kilidokeza chanzo hicho.
Kuhusiana Nsajigwa, licha ya baadhi ya mashabiki kumtaka, lakini wao Simba, wanahofia kiwango chake.

“Hatuwezi kuchukua makapi ya Yanga, afadhali angekuwa Niyonzima (Haruna), sio Ngajigwa!”
Chanzo hicho kiliongeza, bado wako kwenye mazungumzo na beki Juma Nyoso kuangalia kama wamwongeze mkataba kwani kuondoka kwa Kelvin Yondani, kumemfanya apandishe dau.
Katika hatua nyingine, baadhi ya wachezaji wa timu hiyo wakiwemo wapya, wameanza mazoezi.

0 comments:

Post a Comment