Saturday, June 23, 2012

KAMATI ya Uchaguzi ya Klabu ya Yanga SC, jana ilipitisha majina 24 ya wagombea uongozi katika uchaguzi mdogo wa Julai 15, huku wagombea wawili wakichujwa.
Kwa mujibu wa Katibu wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga, Francis Kaswahili, wajumbe wawili waliochujwa kwa kushindwa kutokea kwenye usaili, ni Abdallah Sharia na Jamal Kisongo.

Alisema waliopita kwa nafasi ya uenyekiti ni Yusuf Manji, Sarah Ramadhan, John Jembele na Edgar Chibula huku Ayoub Nyenzi, Clement Sanga na Yono Kevela wakipita kwenye nafasi ya makamu.
Waliopenya kwenye ujumbe, ni Lameck Nyambaya, Ramadhan Kampira, Mohamed Mbaraka ‘Binkleb’, Ramadhan Saidi, Edgar Fongo, Ahmed Gao, Beda Tindwa, Jumanne Mwammenywa na George Manyama.

Wengine ni Gadeuncius Ishengoma, Aaron Nyanda, Omary Ndula, Shaban Katwila, Justine Baruti, Peter Haule na Kevela.
Kaswahili alisema kampeni za wagombea, zitaanza Julai 3, kwa kila mmoja kunadi sera zake juu ya nini atafanya akishinda.

Katika hatua nyingine, usaili ulitawaliwa na vituko mbalimbali vikiwemo vya baadhi ya wanachama kumlaki kwa shangwe mfadhili wao wa zamani, Manji.
Manji aliyefika hapo kwa ajili ya kusailiwa, alijikuta akizingirwa na mamia ya watu waliokuwa wakiimba: “Rais..rais...rais!”
Uchaguzi huo unafanyika kuziba nafasi sita zilizoachwa wazi baada ya watano kujiuzulu kwa nyakati tofauti na mmoja kufariki.

0 comments:

Post a Comment