Sunday, June 10, 2012



Uholanzi na Denmark
William Kvist wa Denmark na Wesley Sneijder wakishindania mpira
Bao la Michael Krohn-Dehli ambalo lilikuwa ndio goli la pekee katika mechi ya kwanza Jumamosi, na ambalo lilifungwa katika kipindi cha kwanza cha mchezo, liliwezesha Denmark kupata ushindi na kuishangaza Uholanzi, ambayo licha ya kupata nafasi nyingi, haikuweza kutumbiza chochote wavuni.
Krohn-Dehli aliweza kuwakwepa walinzi wawili wa Uholanzi na kutia mpira wavuni.

Licha ya Uholanzi kuumiliki mpira vyema, Arjen Robben na Robin van Persie walijivurugia nafasi nyingi za kuibuka washindi.
Robben alikaribia sana kufunga alipogonga mwamba, na Denmark iliponea chupuchupu dakika za mwishomwisho wakati Uholanzi ilidai kwamba Lars Jacobsen alikuwa ameunawa mpira katika lango.

Kocha wa Denmark, Morten Olsen, kabla ya mechi alikuwa amenukuliwa akisema kwamba Uholanzi ni timu bora zaidi kuishinda timu yake, na wengi watayafikiria matamshi hayo yalikuwa ni ya kupimana nguvu kiakili.
Kwa kipindi kirefu katika mechi hiyo ya kundi B katika uwanja wa Metalist, inaelekea kwamba maneno ya Morten Olsen yalikuwa sahihi, kwani timu yake ilionekana kulemewa.

Uholanzi ilionyesha kujipanga vyema, na mchezo stadi na wa kasi, ikiwa na ubunifu mkubwa, na mashambulizi ya mara kwa mara.
Van Persie, ambaye aliifungia klabu ya Arsenal ya England magoli 36 katika msimu uliopita, hakuweza kuiokoa Uholanzi.
Hata hivyo Denmark ilijitahidi vilivyo katika mechi hiyo, ikiongozwa na nahodha Daniel Agger.

0 comments:

Post a Comment