Monday, June 11, 2012
Redds Miss Chang’ombe 2012, Catherine Masumbigana 21, (katikati) akipunga mkono mara baada ya kusimikwa rasmi kuwa mshindi wa taji hilo. Kulia ni mmshindi wa pili, Jesca Haule (18) na Mshindi wa tatu Zulfa Bundala. Masumbigana aliwashinda warembo wengine 13 katika shindano hilo lililofanyika katika Ukumbi wa Quality Center jijini Dar es Salaam Juni 10, 2012.
 Tano bora ya Miss Chang’ombe 2012 ambao wote wamepata tiketi ya kushiriki shindano la Miss Temeke 2012 wakiwa katika picha ya pamoja. Kutoka Kushoto ni Zulfa Bundala (21), Jesca Haule (18), Catherine Masumbigana (21), Miriam Nkisigwa (20) na Flora Kazungu.


 Warembo wakicheza show maalum ya ufunguzi Vazi la ufukwenu, Kutoka kulia ni Restituta Faustiney, Wensley Mabula na Clara Diu.


 Warembo Flora Mayasa (kulia) Catherine Masumbigana (katikati) na Elizabeth Mushi wakiwinda point na vazi la ufukweni.


Mkali wa Bongo Fleva Nassib Abdul 'Diamond' na vijana wake walisindikiza show hiyo kwa kutoa burudani kali jukwaani.


 Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Vijana (Mb) Amos Makala akizungumza jukwaani.


 Wapenzi wa urembo kutoka Chuo Kikuu cha Kampala tawi la Dar es Salaam nao walikuwepo.


 Washiriki wa Miss Ilala 2012 kutoka Kitongoji cha Tabata jijini Dar es Salaam nao hawakukosekana

0 comments:

Post a Comment