Saturday, June 30, 2012

Taarifa zilizotufikia muda huu ni kwamba,Eneo la tegeta Namanga  hali ni tete mara baada ya mmiliki wa sheli za OIL COM kwenda eneo la namanga Tegeta ambapo inasemekana yeye alinunua eneo katika moja ya nyumba za eneo lile ambalo lina makazi ya watu..
Oil com alikwenda pale na watu wake(wabomoji) kwaajili ya kuvunja nyumba zile ili aweze kulichukua neneo lake,hapo ndipo vurugu zilipoanza...kuna watu wawili wanalipotiwa kuumizwa vibaya ambao ni wale waliokuja na OIL COM kwa ajiri ya kuvunja eneo lile.
Wakati tukio hilo likitokea,Msafari wa Rais ulikuwa unapita ukielekea barabara ya Bagamoyo,alipofika eneo la tageta namanga watu ambao inasemekana walikuwa na hasira kali walivamia msafara huo na kuanza kuupiga mawe huku wakizomea.
Askari waliokuwepo pale walifanya juu chini kuhakikisha msafara huo haudhuriki..Hadi nakwenda hewani muda huu Msafara wa Rasi umeshapita,na wale majeruhi walioletwa na mmiliki wa OIL com wamkimbizwa Hospitali kutokana na Kuvuja damu kwa wingi.hakuna kifo kilicholipotiwa kutokea hadi sasa.

0 comments:

Post a Comment