Friday, May 11, 2012
Stori: Mwandishi Wetu, Songea
MTOTO wa ajabu aliyezaliwa hivi karibuni katika Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma, amewasikitisha wengi huku baadhi wakisema hilo ni fundisho kwa wanawake wajawazito .
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Ijumaa, baadhi ya wananchi waliomshuhudia mtoto huyo ambaye sehemu zake za siri ziko kichwani walisema ni tukio la kusikitisha kuwahi kutokea lakini pia iwe ni somo kwa wanawake wajawazito kufuata maelekezo ya wataalamu wa afya.
“Mimi mwenyewe amenisikitisha sana huyu mtoto lakini kwa maelezo kuwa inaweza kuwa imesababishwa na mama yake kunywa dawa zisizostahili kabla ya mimba kutimiza miezi mitatu, basi iwe fundisho kwa wengine la sivyo matukio kama hata yataendeelea kutokea katika jamii zetu.
“Pia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii iangalie namna inavyoweza kumsaidia mtoto huyu kwani anateseka,” alisema Mama Zuhura wa Songea mjini.
Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Mathayo Chanangula alisema kuwa mtoto huyo alizaliwa akiwa na uzito wa kilo 1.9 licha ya kutimiza miezi tisa ya kuzaliwa na kwa kawaida mtoto anatakiwa kuzaliwa na uzito wa kilo 2.5.
Mtoto huyo kila anaponyonya, sehemu yake ya siri ya jinsi ya kiume iliyo kichwani kwake inasimama kama vile anataka kujisaidia haja ndogo.
Gazeti hili linamuombea kwa Mungu mtoto huyo afanyiwe linalowezekana ili arudi kwenye hali ya kawaida.

0 comments:

Post a Comment