Thursday, May 31, 2012

RAIS Jakaya Mrisho Kikwete ameteua wakurugenzi wapya tisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambao pia watakuwa na hadhi ya balozi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam jana na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue, uteuzi huo umeanza Mei 2, mwaka huu.

Walioteuliwa ni Vincent Kibwana ambaye anakuwa Mkurugenzi, Idara ya Afrika; Naimi Aziz (Mkurugenzi, Idara ya Ushirikiano wa Kikanda); Celestine Mushy (Mkurugenzi, Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa); Yahya Simba (Mkurugenzi, Idara ya Mashariki ya Kati), na Bertha Somi ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi, Idara ya Diaspora.

Wengine ni Irene Kasyanju (Mkurugenzi, Kitengo cha Sheria); Dorah Msechu (Mkurugenzi, Idara ya Ulaya na Amerika); Mbelwa Kairuki (Mkurugenzi, Idara ya Asia na Australia) na Silima Haji ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi, Idara ya Mambo ya Nje, Zanzibar.

Kabla ya uteuzi huo, Kibwana alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mkuu; Naimi Aziz (Mkurugenzi Msaidizi), Mushy (Kaimu Katibu wa Waziri Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu), Simba (Afisa Mambo ya Nje Mkuu), na Somi alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mkuu.
Wengine; Kasyanju alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Msechu (Mkurugenzi Msaidizi), Kairuki (Msaidizi wa Rais - Hotuba, Ofisi ya Rais, Ikulu) na Haji alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mkuu.

CHANZO CHA HABARI: Tanzania Daima

0 comments:

Post a Comment