Monday, April 30, 2012



Taarifa ya habari iliyosomwa TBC saa saba mchana wa leo inasema kuwa Mahakama imetengua Ubunge wa jimbo la Sumbawanga Mjini mkoani Rukwa.

Matokeo hayo yametenguliwa katika kesi ya pingamizi la ushindi wa Mbunge huyo iliyofunguliwa na mgombea wa CHADEMA,  Mwalimu Norbet Joseph Yamsebo  kufuatia kasoro zilizojitokeza wakati wa uchaguzi wa mwaka 2010 ikiwa ni pamoja na madai ya kutoa rushwa  kwa makundi mbalimbali ambapo watu wengi walijitokeza kutoa ushahidi na kukiri kuwa ni kweli walipokea vitu kama vile fedha, baiskeli, pikipiki, vinywaji, kinanda kwa Kanisa Katoliki n.k.

Kiti hicho kilichokuwa kikishikiliwa na Aeshi Khalfan Hilaly, CCM, sasa kipo wazi.

0 comments:

Post a Comment