Monday, April 30, 2012


Jana ilikuwa ni siku ya kihistoria kwa msanii aliye hot Bongo kwa sasa na kinara wa tuzo za Kili 2012, 'Diamond Platinum'. Alifanya shoo ya kihistoria kwenye Uwanja wa Taifa wa burudani, Dar Live, uliyoko Mbagala jijini Dar es salaam kwa kwenda na helikopta, akiwa msanii wa kwanza nchini kufanya hivyo. Hapa anaonekana akiwa Uwanja wa Ndege Terminal One akielekea kwenye Helikopta tayari kwa safari
....akisindikizwa na Rubani wake kuelekea kwenye helikopta
....akitoa 'saluti; kabla ya ndege kupaa kuelekea kiwanja cha Dar Live, Mbagala
.....akisali kumuomba Mungu amfikishe salama
...Helikopta ikiwa mita chache juu wa Dar Live ikizunguruka, ambapo Diamond alisalimia mashabiki akiwa angani kwa kutumia 'Wireless Mic'
....Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live unavyoonekana kwa juu
.....Platinum akitua katika uwanja wa Dar Live!
....mashabiki wa Diamond wakionekana kupagawa kwa furaha baada ya kutua na kumuona
...Diamond akiagana na rubani wakati helikopta ikipaa angani, mkononi akiwa ameshika Mic yake
...Helikopta ikiondoka...
....Diamond akiwa ndani ya Mercedes Benz mara baada ya kutua
....Diamond akishuka kutoka kwenye gari tayari kwa shoo...stay tuned!
PICHA: ISSA MNALLY/ERICK EVERIST - GPL

0 comments:

Post a Comment