;

Sunday, February 3, 2013

Sera za Majimbo ni za Lazima! Asiyetaka ahame Nchi!

Unajua kuna kipimo cha ujinga na upumbavu lakini heri mjinga maana anaweza kueleweshwa na mpumbavu katu anajua ukweli ila anaupindisha kwa faida zake

Ridhwan Kikwete na wana CCM wenzie ni moja ya makundi dhaifu kiakili na kihuhalisia, huku kundi linguine la wenye ulemavu wa akili ni baadhi ya wanachadema ambao ni fuata mkumbo, wasiozijua seraza chama chao na hawawezi kuzitetea..poleni!


Faida za sera za majimbo


1. Faida za utawala

Sera za majimbo zinaweza kabisa kufananishwa na Decentralisation system, ambako maamuzi hufanywa na watu wa chini kabisa, kwa jambo husika na kwa wakati husika.

Wananchi wanapewa uwezo wa kujitafuatia uongozi wao, na hivyo kumjweka mtu ambaye anajua mazingira ya eneo hilo, shinda walizonanzo na way forward kuzitatua. Mtu huyu pengine anajua utamaduni wa eneo husika, tabia zao na kupanga mikakati ya kujikwamua kutokana na walivyo.

Kwa kifupi ita improve quality of decision kwa jambo loloye liwe kwa eneo husika kitu ambacho hakipo kwa sasa

2. Faida za uchumi

Mtu yeyote mjinga na asiyeelewa ni yule anayedhani au kufikiri kuwa kuna maeneo nchi hii ni maskini na mengine ni tajiri.

Kansa ya mawazo haya iko kwa viongozi wa CCM na serikali yao wakihubiri kuwa majimbo ni mifarakano na wengine watakuwa maskini
Sema jimbo gani ni maskini, nitakueleza wafanye nini kupata utajiri..

Hakuna kijiji, mkoa au wilaya maskini Tanzania haipo!!! Umaskini ukiwapo ni wa ubongo mdogo wa raia wa mahali hapo

Sera ya majimbo itaharakisha maendeleo kwani ita ‘motivate’ au ku’stimulate brain za watu wa eneo husika kuwaza na kufikiri kipi kifanyike kuleta maendeleo

Wataalamu wa sosholojia wanatanabaisha kuwa, jamii inayotengeneza sere zake, au kuamua mambo yake hufanya kazi kwa bidii ili maamuzi na malengo waliyoyaamua yafikiwe….kwa mfano sera ya kilimo kwanza haitaweza kufanikiwa kwa sababu haijaamuliwa na wananchi na haijaingia akilini au mioyoni mwao ..kwa nini ‘kilimo kwanza’ hata kama sera hii ni nzuri!!

Ni matatizo waliyoyapata akina Nyerere enzi hizo..wakati mpaka leo hii israel ina vijiji ya ujamaa kama alivyoanzisha Nyerere sisi vyetu havipo na kama vipo ni kibahati tu!!

Leo wengi hawajui wilaya ya Mbinga ndiyo tajiri kuliko zote Tanzania kwa kilimo cha kahawa, ufugaji na sasa wanapanda miti!!Nani anajua kuwa mkoa wa mtwara ni wa saba kuliingizia pato taifa?

Au hamjui kuwa wilaya za Ngaka, kiwira zina makaa ya mawe na liganga kuna chuma, nani asiyejua utajiri wa madini na kilimo morogogoro na mazao ya madawa mkoa wa Pwani?

Au nani asiyetamani kuona utajiri za zabibu Dodoma unavuka mipaka na kushindana na Israel ambayo inategemea zabibu kwa sana
Tanzania haina sehemu maskini, J

Juzi Mkongeumeongelewa sana, Mafuta na ziwa ni utajiri wa Kigoma na Rukwa inasifika kwa kilimo…semeni tujue wilaya maskini ni ipi?

Au haiumi kuona Lindi na Mtwara wana gesi ambayo inasafirishwa kuletwa DSM huku wao wakihangaika kucheza ngoma kwa kukosa kazi??

Haiumi kusikia Tanzania ni wazalishaji wakubwa wa dhahabu duniani uku wilaya husika ni maskini wakutupwa, au Almasi ya shinyanga ikiliwa kimya kimya!!! Kweli asali ya tabora na kijani cha Bukoba sio mtaji wa maendeleo ya taifa hili? Nani anabisha??

Sera hii italeta ushindani wa majimbo katika kuongeza kipato cha kaya, kijiji, kata, jimno na taifa!!

Dubai wameweza kuuweka mji wao kuwa sehemu ya kibiashara duniani sehemu ambayo ni jangwa kabisa!!

Kama kuna sehemu kuna jangwa, basi tutaweka DAR LIVE nyingi sana (Ridhwan tenda hiyoo dogo), na starehe nyingine zote ili watu wakipiga kazi ngumu wanaenda kupumzika na kujiburidisha sehemu ambazo zitakuwa haziwezekaniki..japo hamna hizo sehemu

3. Faida za kulinda utamaduni

Hakuna utumwa mbaya na wa kipekee kama kuacha tamaduni zetu, tumeiga wazungu mpaka wanatushangaa, vijana wetu wamekuwa kama mabinti, eti wanabana pua na MASCULINE behavior haipo!!

Malezi duni!!!
Kijana gani leo yuko tayari kupigana na kusema msitu huu wa baba yangu, na yuko tayari kuua simba na kulinda hadhi za kikoo, kifamilia, kikabila na hatimaye taifa??

Sera majimbo japo zimejikita ki-uchumi zaidi, lakini zina faida kubwa sana hata kiutamaduni

Utamaduni wa eneo husika huleta ubunifu wa eneo husika na kuongeza hadhi ya eneo hilo…leo hatuangalii nyimbo za wamasai ila tunanunuA MAKHIRIKHIRI kwa raha zooote huku tukijiona tumeendelea!

Kumbuka pia utamaduni hapa pia ni kurithisha vizazi vijavyo mambo ambayo kizazi cha sasa kinafanya, kama kulima, kufuga nyuki, kuchimba madini , kutengeneza vitu mbali mbali! kurithisha kizazi kijacho.......this is called informal education which is sometime far better than formal education!!

kuna faida gani kumaliza na degree uchwara ya uhandisi wa ujenzi na huwezi kazi wakati kuna fundi aliyejifunza tangu utotoni alianzia kubeba vifaa vya baba yake!!! anajua kila kitu kuliko injinia aliyekuwa na stress za bodi ya mikopo na shida za kukosa vifaa vya mafunzo??


4.
Faida ya kukusanya mawazo

Unapoona mwenzio kaendelea utajiuliza how? Kafanyaje? Maendeleo ya baadhi ya sehemu Fulani Fulani zitaleta ‘data collection’ na mawazo kuwa kwa nini wengine wameendela wanafanyaje fanyaje.

Sera za majimbo zinaweza kupelekea kubadilisha sera za uongozi wa taifa na kufikia kufanya maamuzi ambayo huwezi kuyajutia na una mifano yake.


5.
Kulinda Rasilimali za Taifa

Kumbuka ikiwa kama majimbo yatagawanywa na kuwa mfumo wa states….basi taifa la Tanzania lina weza kuitwa ‘United Sates of Tanzania’ majimbo ambayo yana dola ya local na kitaifa, kulinda maeneo husika.

Ukiwa na mali lazima ulinde mali…kutorosha vitu kama wanyama hakutakuwepo, kuiba michanga ya madini hakutakuwepo, kukata miti ovyo na kuuza kwa bei ya kutupa hakutakuwepo!!! Do I need to say more here??...no!


6.
Kujenga Taifa Imara na viongozi wazuri wa kitaifa


Tuna taifa dhaifu kwa sababu tuna viongozi dhaifu! Tuna viongozi dhaifu kwa sababu tuna taasisi dhaifu, tuna taasisi dhaifu kwa sababu tuna familia dhaifu!


Taasisi kama uongozi wa ngazi mbalimbali ukiwa makini unaleta viongozi makini, taasisi hata za kidini zinaweza kuchochea kupata viongozi wazuri na akina baba wazuri
Ikiwa tyuna kiognozi wa jimbo Fulani aliweka strategy za kupata maendelao na yakaoneka, je hawezi kuwa ndio candidate mzuri wa wizara husika na hata taifa??

Viongozi watakuwa judged na kazi zao za kwenye majimbo na tutakuwa na hakika ya kuwa atafanya jambo akiwa rais let say…sio kuwa na viongozi vimeo kama hawa wasasa ambao haujui katoka wapi, kafanya nini, anaweza nini, unashtukia tu kiongozi na kesho mnalia HAWEZI…kwani nani alisema anaweza??


7.
Mwingiliano wa watu


Uzuri wa sera hizi kwa sababu tunaongelea taifa moja, mtu ataishi sehemua mabayo anajua atazichanga. ‘atatoka’ atatengeneza fedha kulingana na akili zake na ujuzi wake!! Hili huleta maendeleo ya haraka kwa wenye akili! Sio wanaokalia majungu, kuchezabao na kuwaza uchawi!

Sera za majimbo kwa maendeleo ya Taifa, kumbuka kuna limitation zako au hasara zake, japo ni ndogo sana kw ataifa letu change sera za majimbo is not a matter of discussion…is a must!!

8. Kodi husika

Kodi inakatwa kulingana na eneo husika, kwa mfano kodi ya jimbo la Ontario nchini kanada iko tofauti na kodi ya British Columbia japo wako nchi moja, ukasanyaji wa kodi utakuwa rahisi na itafanya kazi iliyokusudiwaLeo hii kaodi zetu hatujui zinafanya nini na haujui umuulize nani! Aibu

9. Watu watapungua DSM (miji mikubwa) ha ha ha ha!!

I hate DSM but I am in!..ila nina kazi yangu na some prospects…ila naona watu wakitaabika, hawajui wafanye nini, hawana future, asubuhi tunajaziana foleni wengine wakiwa na decent jobs wengine hawana na cha ajabu ambao hawana kazi wanaishi maisha mazuri kabisa…sisi wafanya kazi tunakatwa kodi kubwa na ilimradi vituko tupu

Hawa wenyeji wengi waDSM ambao ni jobless ambao wanaweza kwenda elfu arobaini kwenye msiba wa kanumba siku ya kazi asubuhi..wakisikia wenzao mikoani wanazalisha na maisha yao yanaenda vizuri watarudi tu!!

Hata kama wasipoondoka hawa kwasababu wameishalemaa at least tutazuia watu kukimbilia mijini. Maisha ya bahati bahati , maisha yasiyo na muda wala malengo…maisha ambayo unatoka nyumbani saa kumbi na mbili na kufika kazini saa nne!!

Unafikia chai,kucheza karata kufacebook kidogo, lunch na unasinzia kidogo saa tisa unaanza kuangalia usafiri wa kurudi…asilimia 90 ya wafanya kazi wa serikalini ndio wanavyoishi!! Ha ha ha ha!


Watu hukimbilia mijini wakidhani ndiko kuna hela, sera ya majimbo itazuia hili! Japo hatari yake ni kuwa jimbo Fulani kukiwa kuzuri zaidi watu watakimbilia huko….

lakini kama wanazalisha is okay hakuna shida, siyo kama wakazi wa DSM wengi…hawaishi bali wanatafuta maisha!


10.
inatosha

wenu

Waberoya s. Waberoya

N.B huu sio uchambuzi wa sera rasmi ya chadema, maneno rasmi ya sera za chadema kuhusu hili , tafuta sera zake fika ofisi ya chadema iliyo karibu nawe utaipata, hapa nimeelezea tu kwa ufahamu wangu ubora wa sera hii, kumbuka pia kuwa mimi sio mwana chadema wala chama chochote cha siasa.

Viongozi na wanachama 15 wa chadema kutimkia nccr mageuzi kesho
VIONGOZI waandamizi wa Chama Cha Demokrasia
na Mendeleo
CHADEMA pamoja na wanachama 15 wa chama
hicho wanatarajia
kujiunga na Chama Cha NCCR Mageuzi kesho katika
ukumbi wa
Hotel ya Double J jijini Mbeya.

Kwa mujibu wa taarifa za chama hicho zilizotumwa kwa
njia ya ujumbe
mfupi wa simu ya mkononi kwa wanahabari imedaiwa
kuwa viongozi
hao wa CHADEMA watakutana na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya
NCCR-Mageuzi na mshauri wa mambo ya kisiasa Danda Juju ambaye
atamwakilisha, mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho James Mbatia.

Juju ambaye tayari amewasili mkoani Mbeya kwa shughuli hiyo maalum
anatarajia kuwapokea viongozi hao wa CHADEMA ikiwa ni hatua za awali zinazodaiwa kukisambaratisha CHADEMA. Hivi karibuni aliyewahi kuwa Katibu wa Mkoa wa CHADEMA Eddo
Makata alitangaza kujiunga na NCCR-Mageuzi baada ya kujiuzulu kutoka CHADEMA ambapo hata hivyo viongozi wa CHADEMA walidai kuwa walimtimua uongozi na uanachama. Wimbi la mpasuko ndani ya CHADEMA limeanza kuibuka baada ya madai ya kutimuliwa kwa viongozi na wanachama wa chama hicho akiwemo, Makamu Mwenyekiti Baraza la Vijana la Chadema Taifa (BAVICHA)Juliana Shonza na aliyewahi kugombea Ubunge jimbo la Mbozi Mashariki Mtera Mwampamba.

Hoja binafsi ya @HKigwangalla ya mfuko wa mikopo ya vijana kwenye kilimo

HOJA BINAFSI YA KULITAKA BUNGE LIPITISHE AZIMIO LA KUANZISHA MPANGO MAALUM WA KUKUZA AJIRA KWA VIJANA KWA KUANZISHA MFUKO WA MIKOPO YA VIJANA WANAOWEKEZA KWENYE KILIMO NA VIWANDA VYENYE UHUSIANO WA MOJA KWA MOJA NA KILIMO

Mhe. Spika, awali ya yote nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu muumba wa viumbe vyote, aliyetujaalia pumzi na kutupa afya safi, nguvu na uwezo wa kufika hapa siku hii ya leo, na zaidi kuniwezesha mimi kupata fursa hii adhimu na adimu sana kuwasilisha hoja hii mbele ya Bunge lako tukufu.

Mhe. Spika, nakushukuru sana wewe binafsi, naibu wako, wenyeviti wa Bunge na makatibu kwa msaada wenu katika kuwezesha uwasilishaji murua wa hoja hii siku ya leo. Kwa namna ya kipekee namshukuru sana Mhe. Jenista Mhagama (Mb.), Katibu wa Kamati ya Wabunge wa CCM kwa ushauri na ushirikiano alionipa wakati nikiandaa hoja hii, pia bila kumsahau Mhe. Hussein Mzee (Mb.), Mtunza Hazina wa Kamati ya Wabunge wa CCM, na watumishi wote wa Ofisi yetu ya Kamati ya Wabunge wa CCM.

Mhe. Spika, naomba pia nitumie fursa hii kuwashukuru wananchi wa Nzega kwa kuendelea kuniunga mkono katika harakati zetu za kuleta mapinduzi ya kiuchumi na kijamii Nzega. Wananzega ni mashahidi na wafaidika wakubwa wa miradi ya kilimo cha pamba, alizeti, miembe ya kisasa ya SUA, na sasa tunaingia kwenye uzalishaji na ufugaji wa kuku, miradi ambayo ilibuniwa kwa ushirikiano baina ya wananchi wa Nzega na Mbunge wao, Dkt. Hamisi Kigwangalla, ambaye ni Mwenyekiti Mwanzilishi wa Shirika la Maendeleo Nzega (yaani Nzega Development Foundation Ltd), kwa kutumia nadharia zinazofanana na mapendekezo ya kwenye hoja hii. Ujumbe wangu kwa wananchi wa Nzega ni kwamba, nawaomba msitetereke pamoja na jitihada za wapinzani wangu kisiasa kupotosha ukweli, jambo ambalo halijawahi kufanikiwa – ni imani yangu kwamba ‘nyie wenyewe mnaijua dawa yao.’

Mhe. Spika, kazi ya ubunge ni ngumu sana, ina changamoto nyingi. Kubwa kwa mbunge kijana kama mimi ni ‘muda’. Muda wa kusoma, muda wa kuzaa, muda wa kulea na muda wa kutekeleza majukumu ya kiwakilishi. Niwashukuru mke 
wangu Dr. Bayoum (na nimpe pole kwa uchungu anaoupata huko labour ward), na mabinti zangu Sheila na Hawa Kigwangalla kwa kuendelea kunivumilia kila siku ninapokuwa ‘bize’ kutekeleza majukumu yangu. Wote nawaomba wadumishe upendo na uelewa kwangu wakitambua kuwa ninawapenda na mara zote ninawakumbuka sana, ninawa-‘miss’ sana!

Mhe. Spika, ama baada ya shukrani naomba sasa nianze kuiwasilisha hoja yangu rasmi kama ifuatavyo: Kwamba, japokuwa katika kipindi cha miaka 15 iliyopita Tanzania imerekodi viwango vya juu sana vya kukua kwa uchumi, tuna mafanikio kidogo sana katika kupunguza umaskini wa kipato kwa wananchi; na pia ukuaji huu mkubwa wa uchumi umeshindwa kuzalisha ajira za kutosha kuendana na kasi ya kuongezeka kwa idadi ya vijana kwa sababu za mpito za kidemografia (demographic transition), na pia ukuaji huu wa uchumi umeshindwa kuendana na ukuaji wa idadi ya vijana wanaotafuta kazi za kuajiriwa na pia kujiajiri, pia ukuaji huu wa uchumi unaopigiwa mfano kila kona ya dunia hii bado umeshindwa kuendana na kukua kwa kasi ya wahitimu kutoka kwenye vyuo vya elimu ya juu, ya kati na hata vile vya ufundi na ujuzi mbalimbali, na pia ukuaji huu umeshindwa kuendana na kukua kwa lazima kwa kasi ya uhitaji wa kilimo cha umwagiliaji kutokana na kupungua kwa ujazo wa mvua zinazonyesha na hivyo kupelekea wakulima wadogo vijijini wanaotegemea mvua, kupata mazao pungufu ya matarajio na jitihada zao.

Mhe. Spika, Uchumi wa Tanzania umekuwa ukikua kwa wastani wa asilimia 7 kwa kipindi cha kuanzia 2001 – 2010, ulianguka kidogo mwaka 2009 ambapo ulishuka mpaka asilimia 6 (kwa sababu ya kuanguka kwa uchumi wa dunia), japokuwa uliruka juu tena na kurudi kwenye kiwango chake cha awali cha asilimia 7 mnamo mwaka 2010. Sekta zilizokua kwa kasi zaidi mwaka 2010 zilikuwa ni mawasiliano (asimilia 22.1), ikifuatiwa na ujenzi (asilimia 10.2), umeme na gesi (asilimia 10.2), fedha (asilimia 10.1) na uzalishaji viwandani (asilimia 7.9). Kwa ujumla kukua kwa pato la taifa kuliendeshwa zaidi na biashara (trading), huduma za marekebisho (repairs), kilimo, uzalishaji, biashara ya majengo (real estate business) na huduma za kibiashara (business services). Mfano katika kipindi cha kuanzia 2001 mpaka 2007, pato la taifa lilikuwa kwa kiwango cha wastani wa asilimia 7.1, umaskini ulipungua (kwa kipimo cha Head Count Index) kutoka 35.7 mpaka 33.6 tu. Hii inaonesha wazi kabisa kwamba ukuaji wa uchumi haujawa mpana na haujawalenga wananchi maskini.

Mhe. Spika, kwa mujibu wa takwimu za Integrated Labour Force Survey za Tanzania za mwaka 2006, kiwango cha ujumla cha ukosefu wa ajira kilikuwa ni asilimia 12.9; kwa vijana kiwango ni kikubwa zaidi ya hiki, ambapo ni asilimia 17 kwa Tanzania Bara na asilimia 20 kwa Zanzibar. Hii inaonesha kuwa nguvu kazi kubwa zaidi ya Taifa letu haitumiki ipasavyo (underutilized), inaachwa inachanganyikiwa. Hata hivyo, viwango hivi bado ni vya chini ukilinganisha na ongezeko kubwa la vijana wanaohitimu masomo kutokana na wimbi kubwa la ongezeko la vyuo vikuu katika kipindi cha kuanzia mwaka 2006 hadi sasa. Na pia hata wale ambao wanachukuliwa kama wameajiriwa kwenye sekta binafsi, na ama wamejiajiri kwenye biashara ndogo ndogo, ufundi, kilimo, mifugo na uvuvi, kumekuwa hakuna tija ya kazi wanayoifanya. Mhe. Spika, Inakadiriwa kwamba kila mwaka zaidi ya wahitimu 1,200,000 kutoka kwenye ngazi mbali mbali za taaluma wanaingia kwenye soko la ajira lakini soko hili lina uwezo wa kuhudumia wahitimu 200,000 tu!

Mhe. Spika, tunatakiwa tufike mahala tukae chini tujiulize, tutafakari, na hatimaye tuchukue hatua. Kwa takwimu hizi utaona kuwa, kunyanyua juu kiwango cha ukuaji wa uchumi na haswa kwenye sekta zinazoshirikisha watu wengi zaidi ni jambo lenye umuhimu wa kipekee, hivyo kuvutia na kuwezesha uwekezaji kwenye sekta ambazo zinaajiri watu maskini walio wengi ni jambo la lazima.

Mhe. Spika, Takriban Miezi 13 iliyopita, ndani ya siku moja, nilikutwa na wakati mgumu sana baada ya kupokea ujumbe kutoka kwa vijana mbalimbali 6 waliohitimu masomo yao ya shahada mbalimbali wakinitaka niwasaidie kupata mahala ‘pa kujishikiza’, kwenye mashirika ya 'marafiki zangu'. Mtihani huu ulikuwa mgumu sana kwangu. Nilijiuliza, ‘Nitautatuaje?’ Imani yangu ni kwamba siko peke yangu katika hili. Waheshimiwa wabunge wenzangu ni wahanga wa maswali magumu kama haya kutoka kwa vijana majimboni kwetu. Matumaini ya vijana na ya watanzania (kwa ujumla) yamewekwa rehani kwenye vichwa na mioyo ya waheshimiwa wabunge.

Mhe. Spika, binafsi nilibaki nikijiuliza, ‘Hivi marafiki zangu kila siku wanatoa nafasi za ajira kwenye mashirika yao?’ Maswali haya yalinifanya nimfikirie upya kijana wa kitanzania. Nikapata muda wa kufikiri kwa mapana na kwa kina kidogo na kubaini kwa haraka tu kabisa, na bila shida hata kidogo; kwamba, kama Taifa tuna tatizo, tena tatizo kubwa kweli kweli: nilijiuliza sana, hivi ni kwa nini vijana hawa hawakunijia na mawazo ya namna ya kujiajiri badala yake wanataka mahali pa kujishikiza? Tunazalisha ajira ngapi kwa mwaka? Wanaohitimu na wanaotafuta ajira, kutoka kwenye utitiri wa vyuo vikuu, kwa ujumla wao wapo wangapi? Wanaobaki bila ajira na ni wenye nguvu, nia, ari na wasaa wa kufanya kazi ni wangapi? Na je kama taifa tunawatumiaje?

Mhe. Spika, leo hii kuna fursa za masoko kwenye nchi za SADC, EU, AGOA na Jumuiya ya Africa ya Mashariki. Leo hii ni vijana wangapi wa kitanzania, kwa mfano, wamepata ajira nchini Kenya ama na kinyume chake ni vijana wangapi wa Kenya wanavamia soko la ajira la Tanzania na wanapewa nafasi za kipaumbele kwenye mashirika mbalimbali binafsi? Ni kampuni ngapi za vijana wa kitanzania zinauza bidhaa zake nchini Kenya? Tunapofungua milango kwa kusaini na kuridhia mikataba mbalimbali ya kikanda na kimataifa, maana yake tunawakaribisha wenzetu ndani ya soko letu, je sisi tunaingia kwenye masoko yao? Ni lazima tufanye jitihada za maksudi za kuwaandaa vijana wa kitanzania kuwa washiriki mahiri, kuwa washindani wenye nguvu kwenye masoko ya ajira na kwenye kunyakua fursa mbali mbali za kuuza bidhaa nchi za nje.

Mhe. Spika, tunaposema uchumi wetu umekua, tunatathmini kama kweli kukua huko kumetupa faida kiasi gani? Tunapata faida gani kutokana na kuongezeka kwa vyuo vikuu, taasisi za kuzalisha fikra (think tanks) na kukua kwa idadi ya wasomi wetu (critical mass)? Je tumejiandaa kiasi gani kukuza ajira kwa vijana wetu? Maswali haya na mengi mengineyo ni magumu na hayajibiki kirahisi hata kidogo!

Mhe. Spika, nikasema, labda tuanzishe mjadala mahsusi wa kitaifa, utakaolitazama suala la ajira kwa vijana wa kitanzania kwa mapana na marefu, na kulipatia ufumbuzi. Vijana wa zama hizi hawataki maneno, wanataka vitendo. Maneno na mipango mizuri iliyoandikwa haitowasaidia sana, wanahitaji fursa nzuri za ajira, za kujiajiri, za kuendesha maisha yao. Mipango mgando na butu kama ule wa kuwawezesha vijana kupitia mfuko wa maendeleo ya vijana kule kwenye halmashauri zetu, ama ule wa shirika la kuhudumia viwanda vidogo vidogo (SIDO) haijaleta mapinduzi yoyote yale mpaka sasa. Hakuna mtu mwenye akili timamu anayeweza kusimama hapa na kuipigia jalamba mikakati kama ile maana vijana hawaielewi na wala hawajaona matunda yake. Tena vijana wa siku hizi, Mhe. Spika, hawako tayari kutumiwa na wanasiasa, wa chama chochote kile cha siasa kwa faida za kisiasa. Vijana wanataka kuona mabadiliko, wanataka kuona mapinduzi, si yale ya kisiasa yasiyo na tija, wanataka kuona mapinduzi ya kiuchumi, na wako tayari kushiriki katika harakati za kufikia mapinduzi hayo.

Mhe. Spika, nimefanya tafakuri tunduizi juu ya ufumbuzi wa tatizo la ajira kwa vijana na pia kukuza uchumi wa nchi yetu na nimebaini kwamba uwekezaji kwenye kilimo na viwanda vyenye uhusiano wa moja kwa moja na kilimo ndiyo suluhu ya haraka na ya ukweli ya tatizo la ajira kwa vijana; kwa namna yoyote ile haimaanishi hata kidogo kuwa hoja hii ndiyo muarobaini wa tatizo hili, ambalo ni pana na linahitaji ufumbuzi mpana zaidi wa kila sekta na linahitaji ushiriki wa wadau wengi zaidi, na kwamba si lazima kuwa vijana wote watataka kuwekeza kwenye ‘industries’ nilizozitaja hapa, hii ni dira tu na ni mchango wangu mdogo kwenye kutafuta ufumbuzi wa tatizo hili kabla halijawa ‘janga la kitaifa.’

Mhe. Spika, vijana wenye nguvu, wasipotumika vizuri, watatumiwa vibaya na watu wajanja wajanja wenye uchu na tamaa ya madaraka. Na wao wenyewe wanaweza kujiingiza kwenye vitendo visivyofaa, kama kwenye mitandao ya biashara haramu za madawa ya kulevya, mitandao ya madangulo ya ukahaba, na hatimaye kuangamia wao wenyewe na wenzao wengine wengi zaidi. Kama taifa tuna wajibu wa kuandaa mazingira wezeshi kwa ajili ya kizazi cha mbele yetu. Swali lingine hapa linazalishwa, Je tunaandaa mazingira hayo?

Mhe. Spika, azimio hili likitekelezwa litawawezesha vijana wote, wasomi na wasio wasomi, bali wajasiriamali, wenye ari, mshawasha, nia, tabia, fikra, hekima, utayari, utashi sahihi, na pia nguvu za kuwa watengeneza ajira badala ya watafuta ajira (job creators instead of job seekers) wajiunge kwenye vikundi na wafanye kazi za kujiajiri kwanza wao wenyewe lakini pia watakuwa waajiri wa wenzao. Mbali na faida za kiuchumi zitakazopatikana, pia mpango huu utaamsha ari ya mabadiliko ya kifikra (mindset change); kwamba badala ya vijana kusoma huku wakitarajia ajira baada ya masomo, kama ilivyo ada, watakuwa wakisoma huku wakifikiria kujiajiri na kutajirika, badala ya kuishi na kukua wakitegemea serikali itawaletea maendeleo yao, vichwa vyao sasa vitafunguka wataweza kufungulia ‘potentials’ zao nyingine, wataanza kuota kufika mbali zaidi katika maisha yao. Na wale watakaofanikiwa watakuwa mfano bora zaidi kwa wenzao, na hapo tutajikuta tumejenga taifa la watu makini, wawajibikaji na wenye tamaa ya mafanikio (ambitious na responsible citizens). Ile dhana kwamba utajiri si stahiki yao, ni wa watu wachache tu wenye asili hiyo, kwa hakika itatoweka!

Mhe. Spika, Pamoja na kuwekeza kwenye kilimo, vijana wataweza kujenga na kuendesha viwanda vyenye uhusiano wa moja kwa moja na kilimo (backward linkage), pia wengine wataanzisha kampuni za masoko (marketing & trading), wengine za usafirishaji (logistics and handling of goods), pia wataanzisha viwanda wezeshi (associated industries) mfano vya ‘packaging materials’.

Mhe. Spika, wakati wengine wakiendeleza mashamba na viwanda vyao, ajira zitajizalisha zaidi kwenye sekta nyingine kutokana na uwekezaji huu (multiplier effect): mfano, wakati wengine wanawekeza kwenye mashamba na kwenye viwanda vyao, wengine watakuwa wanawekeza kwenye kuanzisha makampuni ya kutoa ushauri kwa wakulima, wengine kwenye ugunduzi wa mbegu, uzalishaji na usambazaji wa mbegu bora, wengine kwenye habari na mawasiliano (mf. Kuboresha kilimo na upatikanaji wa masoko na taarifa za bei kwa kutumia njia za kisasa za mawasiliano kama vile ujumbe mfupi wa maneno (sms), intaneti – wengine wakiwatengenezea wengine tovuti kwa ajili ya biashara zao.

Mhe. Spika, pamoja na kuongeza tija na ufanisi (productivity and efficiency), tutakuwa tumeongeza uzalishaji wa mazao na bidhaa zinazotokana na mazao, tutakuwa tumeleta uhakika wa masoko ya mazao ya wakulima karibu zaidi na wakulima (market stability and sustainability) na hatutouza mazao ambayo hayajaongezwa thamani kutoka shambani. Matarajio yangu ni kwamba, tutakuwa tumetatua si tu tatizo la ajira kwa vijana bali pia kwa kiasi kikubwa la kiuchumi kwa kuongeza uzalishaji, kuongeza thamani ya mazao yetu, kuhakikisha masoko ya uhakika kwa wakulima, na mwishowe kupunguza kiwango cha mfumuko wa bei (inflation rate) ya vitu na zaidi kuongeza mauzo ya bidhaa zetu nje ya nchi na kupunguza manunuzi ya bidhaa kutoka nje ya Tanzania, jambo ambalo litachangia kwa kiasi kikubwa kuimarisha akaunti yetu ya ‘balance of payments’.

Mhe. Spika, ukiuangalia mpango huu vizuri utagundua kwamba kutakuwa na vijana wasomi (watakaowezeshwa kuwekeza kwenye mashamba makubwa ya kibiashara na viwanda) na wale ambao hawajasoma (watakaowekeza kwenye kilimo cha mashamba ya saizi ya kati na hata yale madogo madogo, na pia viwanda vidogo vidogo), haya makundi yatabebana kwenye model hii, na hivyo kila kundi litatoa ajira kwa watu wengi zaidi.

Mhe. Spika, kama kila kitu kikienda sawa (ceteris paribus), kibaiolojia tunawategemea vijana wataishi kwa muda mrefu huko mbele zaidi ya wazee. Tukiwatumia vijana kwa kuona mbele kuna nini, wakiwekeza leo na wakifanikiwa kuendesha biashara zao kwa faida maana yake ni kwamba baada ya miaka 20, Tanzania itakuwa na watu wenye nguvu na wenye uchumi imara, na kwa kuwa sekta binafsi ni injini ya kukua kwa uchumi wa nchi, tutatoka kwenye kundi la nchi maskini zaidi duniani. Pia, ni rahisi sana kwa kijana kufanya jambo la kubahatisha ama kuthubutu (kubeba ‘risk’) na kufanya kazi kwa bidii kufikia ndoto zake bila wasiwasi, na zaidi kundi hili likipewa kipaumbele linaweza kuondoa utamaduni wa watanzania kutoka kwenye kufanya mambo kwa mazoea (yaani 'business as usual' na 'laissez-faire') na kuwa nchi ya watu wenye kufanya kazi kwa ubunifu wa hali ya juu na ‘passion’ ya ukweli. Mimi naliona hili ndiyo kundi pekee litakaloweza kuijenga Tanzania mpya, Tanzania ya miaka 20 ijayo. Sina nia ya kuonekana ni mbaguzi wa wazee, ama simaanishi kuwa wazee hawahitajiki, la hasha, napenda kusema tu kuwa mpango huu ni mahsusi kwa vijana tu.

Mhe. Spika, ni lazima tuwe na ndoto. Na pia ni lazima tujipange kuzifikia ndoto zetu. Hakuna ujanja mwingine. Hatuwezi kufanikiwa kwa kutumia mikakati ile ile iliyotufikisha hapa. Ni jambo moja kuwa na ndoto, na ni lingine kujipanga namna ya kuifikia. Ni jambo lisiloyumkinika kupanda bangi na kujiandaa kuvuna mchicha hatimaye! Tunahitaji kubadilika, tupande mbegu za kuuandaa uchumi wa Tanzania ya kesho. Tunahitaji mawazo mapya , njia mpya za utekelezaji, na hapo ndipo tutaona matokeo mapya!
Mhe. Spika,

Baada ya maelezo haya, hoja yenyewe sasa inawasilishwa, kwa mujibu wa Kanuni ya 54 (1.), (2.) na (3.), kama ifuatavyo: -

KWA KUWA, idadi kubwa ya wananchi wa Tanzania (zaidi ya asilimia sitini) ni vijana chini ya miaka 40
NA KWA KUWA, vijana hawa ni nguvu kazi ya kutegemewa katika nchi yetu na kama kila kitu kitabaki sawa (ceteris paribus), kibaiolojia vijana hawa watakuwepo nchini kwa miaka mingi ijayo ukilinganisha na wazee

NA KWA KUWA, vijana wanahangaika kutafuta ajira na kuna fursa nyingi za kutengeneza ajira nchini ambazo hazijafanyiwa kazi

NA KWA KUWA, vijana wengi nchini humu wamedhihirisha kuwa wana ari, nguvu, nia, elimu, ujuzi na vipaji vya kupigiwa mfano kwenye fani mbalimbali na wanakosa mitaji na mpango mahsusi na wa maksudi wa uwezeshi, wanahitaji uongozi (leadership, mentorship and guidance) ili kukamilisha ndoto zao

NA KWA KUWA, tuna malengo ya kuivusha nchi yetu kiuchumi kufikia 2025 (cf. dira ya maendeleo Tanzania 2025) kuelekea nchi zenye uchumi wa ngazi ya kati (MICs), wengi wa watakaokuwepo (kibailojia) watakuwa ni vijana, na wanatakiwa kuwezeshwa ili wawe mhimili wa mwenendo wa uchumi wa Tanzania ya kesho tunayoilenga, na pia wakiwezeshwa leo tunaamini ndiyo wataifikisha Tanzania huko tunapopataka kesho

NA KWA KUWA, ili kuzalisha ajira nyingi zaidi na kwa haraka, kilimo na viwanda vyenye uhusiano wa moja kwa moja (backward linkage) na kilimo ndiyo jibu la msingi la nia hiyo

NA KWA KUWA, ilani ya uchaguzi ya CCM (Uk. 88 - 95, Kifungu Cha 79 (i.), (ii.) na (iii.)), ambacho ni Chama kinachotawala nchi yetu, inatambua na kutoa maelekezo mazuri kabisa kwa serikali kuhusiana na hoja hii ya kukuza ajira kwa vijana, na pia Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano (cf. Uk. 92, kifungu cha 5.2.4), na MKUKUTA II vinatambua umuhimu wa kutekeleza haya. Pia Mhe. Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwenye maelezo yake ya utangulizi mwanzo wa Mpango huo anasema na ninamnukuu hapa, kwamba “Employment creation, particularly for the youth, is also a critical cross-cutting target of this Plan.” [inatafsirika Kiswahili kama ‘kutengeneza ajira, hususan kwa vijana, ni lengo mtambuka la huu mpango’]. Kinachotakiwa sasa si kingine bali ni kufanya jitihada za utekelezaji tu maana barabara zote zinaelekea huko.

HIVYO BASI, bunge linaazimia kuitaka serikali yetu ifanye yafuatayo:
 1. KWAMBA, Ianzishe mpango maalum wa kukuza ajira kwa vijana kwa kuanzisha mfuko wa mikopo ya vijana wanaowekeza kwenye kilimo na viwanda vyenye uhusiano wa moja kwa moja (backward linkage) na kilimo. Mfuko huu hapo baadaye utaendelezwa na kuwa Benki ya Maendeleo ya Vijana Tanzania (Tanzania Youth Development Bank).

 1. KWAMBA, Ianzishe mfuko maalum wa kutoa mikopo ya uwekezaji kwa vijana wa Tanzania, utakaoitwa ‘Tanzania Youth Enterprise Challenge Fund’ na iwekeze katika mfuko huu mtaji usiopungua bilioni za kitanzania mia mbili (mwaka wa kwanza) na bilioni mia moja kila mwaka wa fedha utakaofuata. Mfuko huu uwalenge vijana watakaowekeza kwenye sekta ambazo tutazichagua, sana sana tuweke kipaumbele kwenye sekta za kilimo na viwanda vyenye uhusiano wa moja kwa moja (backward linkage) na kilimo ili kuzalisha ajira nyingi zaidi kwa vijana. Vijana hawa waingizwe kwenye mashindano ya kuandika maandiko ya miradi (project proposals/business plans), na ile itakayoshinda kwenye mchakato huu ndiyo pekee itakayochaguliwa. Mchakato huu katika hatua Fulani, kama itabidi iwe hivyo, uwashirikishe wananchi kwa njia ya kupigia kura miradi wanayoona inafaa na ushindi katika hatua hii iwe ni kigezo kimojawapo cha kuwapata watakaoshinda.
 NA KWAMBA, Mikopo itakayotolewa katika mchakato huu itakuwa ni yenye masharti nafuu, kama ifuatavyo:
 • Itakuwa na riba ndogo (asimilia 6 kushuka chini),
 • Itakuwa na kipindi kirefu cha kurudisha (payback period)  - cha takriban miaka 15-20,
 • Itakuwa na kipindi kirefu cha kutoanza kurudisha mkopo (grace period) – kati ya miaka miwili hadi mitatu
 • Isiwe na masharti ya dhamana/security za mali (maana vijana hawana assets zozote) bali iwe na ‘dhamana’ maalum kama cheti cha elimu/ujuzi kwenye fani husika, ardhi ya shamba lililorasimishwa kwa utaratibu unaokubalika, na iwe kwenye usimamizi wa kitengo maalum cha mfuko huo. Mpango huu uendane na kuweka utaratibu mzuri na rahisi wa kusajili mashamba na ardhi.

 1. KWAMBA, Itenge maeneo maalum ya kuwekeza (special economic zones) chini ya mpango huu. Ichague maeneo maalum kwa mazao na viwanda maalum kwenye wilaya mahsusi za nchi yetu. Vijana waelekezwe na kusimamiwa kuwekeza kwenye sekta zilizochaguliwa na wawezeshwe kupata mitaji hiyo. Uanzishwaji wa miradi hii uendane na kuwepo kwa sharti la kuwataka vijana (wawekezaji) kuhamasisha kilimo cha kisasa na kusaidia wakulima kwenye maeneo yanayowazunguka kwa njia ya mkataba maalum (contract farming) wa kukopesha pembejeo za kilimo, mbegu bora za mazao, zana za kilimo ama kuwalimia na kuwavunia kwa mashine, kutengeneza mifumo ya umwagiliaji – hii itasaidia kuongeza tija na ufanisi kwa wakulima.
 2. KWAMBA, serikali iamue kuchagua sekta zitakazohusika kwenye mpango huu maalum kwa ajili ya vijana. Baadhi ya sekta za kuangaliwa ni pamoja na kilimo kikubwa cha kibiashara cha umwagiliaji – kila mradi ni lazima uwe na mpango wa kuwafikia wakulima wadogo wanaozunguka shamba husika (satellite out-grower schemes), ujenzi wa viwanda kama vya kuchambua pamba (ginneries) na kusokota nyuzi (spinning); kukoboa na kusaga unga/chakula cha mifugo; kukamua na kusafisha mafuta ya kula, pia kutengeneza sabuni; kusindika juice n.k, utafanyika kwenye maeneo ya karibu na mashamba hayo. Kila eneo la mradi litengwe likiwa na uwezekano wa kufanya utanuzi kwenye sekta hiyo ili kukamilisha mnyororo wa thamani kwenye  eneo moja (value chain).
Mhe. Spika,
NAOMBA KUTOA HOJA.Dr. Hamisi Kigwangalla (MB),
Jimbo la Nzega. 

Ngwala aka Kata-Funua

Picture
Wanafunzi wasanii wa Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa akifanya onesho la igizo la mfano wa vijana wanaokosa elimu huishia kushiriki katika matukio ya uhalifu katika hafla ya kuwaaga wanafunzi wa Kidato cha Sita shuleni hapo ambayo mgeni rasmi alikuwa Mhe. Edward Lowassa (picha: Nyakasagani Masenza)

Lowassa na Elimu: Kuna udhaifu mkubwa unaosababishwa na mitaala mibovu

Wakati hatma ya ubunge wa Mbunge wa Kuteuliwa, James Mbatia (NCCR-Mageuzi) ikisubiriwa kama alivyoahidi, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amejitokeza akionesha kuunga mkono hoja ya Mbunge huyo kuhusu mitaala.
Akiwa bungeni wiki hii, Mbatia alisema Serikali haina mitaala ya elimu na kama itaweza kuiwasilisha bungeni, yeye atakuwa hana budi ila kujiuzulu ubunge.

Serikali kwa upande wake kupitia Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa, iliahidi kupeleka nakala 300 za mitaala hiyo ili igawiwe kwa wabunge na kuthibitisha madai ya Mbatia kuwa ni batili.

Wakati Serikali ikitoa ahadi hiyo, Mbatia alisimamia hoja yake, akisema Wizara haina mitaala na akaahidi dhahiri kwamba iwapo itaoneshwa, atakuwa tayari kujiuzulu ubunge.

Katika hatua nyingine, Lowassa katika mahafali ya 13 ya sekondari ya Benjamin Mkapa, Dar es Salaam jana, akiwa mgeni rasmi, alisema kuna udhaifu katika elimu nchini kutokana na mitaala mibovu ambayo inaandaa wahitimu kutafuta na si kutengeneza kazi.

“Ubovu wa mitaala ya elimu unawatengeneza kuwa watafuta kazi, lakini ni vema zaidi mitaala ikabadilishwa, ili hata wahitimu wanapomaliza masomo yao wawe watengeneza kazi na si tegemezi tena,” alisema Lowassa.

Alisema mitaala inahitaji kubadilishwa ili kusaidia wanafunzi wawapo shuleni na wamalizapo wajiendeleze kimaisha kwa kutengeneza kazi zao binafsi.

Wakati hayo yakiendelea, wabunge wa upinzani waliazimia kupeleka taarifa kwa Mamlaka ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge  kutaka Waziri Kawambwa  ajiuzulu kwa kudanganya Bunge au Mamlaka iliyomteua imfukuze kazi.

Katika Mwongozo wa Spika  juzi, baada ya malumbano yaliyosababisha yeye na wabunge wa upinzani kususa Bunge, Mbatia alitaka Waziri Kawambwa awasilishe nakala siku hiyo ili kujiridhisha nani alisema uongo.

“Nilitamka rasmi, kwamba kama ipo (mitaala) niko tayari kuondoka katika nafasi hii,” alisema Mbatia.

Akitoa Mwongozo, Naibu Spika Job Ndugai alisema: “Kwa dai lake anaomba Mheshimiwa Waziri Kawambwa alipokuwa anachangia hoja yake kijitabu alichokionesha kuhusu mitaala, alitaka kiwekwe mezani.”

Ndugai aliendelea: “Na uhakika kutoka serikalini ni kwamba Mheshimiwa Waziri ameshaagiza Dar es Salaam kutoka kwa wachapaji, nakala 300 kwa ajili ya  wabunge na zitaletwa Februari 6, wiki ijayo…mitaala hiyo itakuwa katika ofisi ya Bunge; naomba subira tutafika mahali tu pa kuelewana.”

Mbatia katika hoja yake alisisitiza kwamba hadi mwaka 2011, nchi haikupata kuwa na mitaala rasmi ya kitaifa kwa ajili ya elimu ya shule za msingi au sekondari.

Alisisitiza kwamba, hapajawahi kuwapo andiko mahsusi la mtaala wa elimu kwa taifa na kusema Taasisi ya Elimu imekuwa ikiajiri wakuza mitaala kwa zaidi ya miaka 15 bila kutoa mitaala yoyote katika namna ya andiko mahsusi.

Kwa mujibu wa Mbatia, nyaraka za Wizara ya Elimu zina ainisho la dhana ya mitaala ambalo kwa kiasi fulani linatoa mtazamo usiowezesha kutambua mitaala inayotakiwa kuwapo kwa mapana.

Waziri Kawambwa alipokuwa akijibu hoja juu ya mitaala, alisisitiza kwamba ipo na tangu nchi ipate uhuru, imebadilika mara nne na kutaja miaka ya mabadiliko kuwa ni 1967, 1979, 1997 na 2004-2009.

Mjadala kuhusu mitaala ulijitokeza kutokana na hoja binafsi ya Mbatia bungeni Alhamisi kuhusu udhaifu ulio katika sekta ya elimu nchini.

Kwa upande wake, Lowassa  alisema kuna udhaifu mkubwa katika sekta ya elimu nchini, unaosababishwa na ubovu wa mitaala.

Alikitaka Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kuacha kugombana na Serikali badala yake kikae ili kukubaliana jinsi ya kutatua migogoro baina yake na Serikali.

“Elimu isaidie wahitimu kutengeneza kazi, kwa sababu nchini hakuna ajira na kama hakuna matokeo yake ni mabomu kulipuka, kwa mfano wa Misri, sasa tusipokuwa makini na hapa kwetu yatalipuka mabomu ya aina hiyo,” aliongeza.

Aliipongeza hatua ya Serikali kurudisha mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa wanafunzi wanaohitimu kabla ya kuendelea na vyuo vikuu, huku akiwasisitiza wanafunzi kuwa mafunzo hayo yatawajengea utaifa na uzalendo wa nchi yao hivyo wasiwe na wasiwasi.

“Maombi yalikuwa ni vijana 40,000 lakini kwa sasa Serikali imepeleka vijana 5,000, kwa mwakani ihakikishe inapeleka vijana wote,” alishauri.

Aidha, aliongeza kuwa wanafunzi hao wamepata bahati ya kumaliza katika shule yenye jina kubwa - Benjamin William Mkapa - ambaye alikuwa Rais wa Awamu ya Tatu, aliyeongoza nchi kwa uadilifu mkubwa na kuacha nchi ikiwa ya amani na mshikamano kwa Tanzania Bara na Visiwani.

“Mkapa alikuwa kiongozi shujaa, alikuwa muwazi na mkweli na mpaka sasa bado ni shujaa kwani kutokana na uongozi wake, alikuwa msuluhishi wa migogoro ya nchi mbalimbali,” alisema Lowassa.
Shukurani kwa: Picha (zote) blogu ya Nyakasagani; Taarifa ya maandishi blogu ya Ziro99

Moto katika majengo ya PPF, Dar es Salaam

.
Picha ya jengo la PPF ikionesha moshi mkubwa unaofuka kutoka kenye jengo hilo (Shukurani ya picha: A, rafiki wa M.C.)

Taarifa zafahamisha kuwa, huenda hitilafu ya umeme iliyotokea kwenye mitambo ya mawasiliano iliyopo katika chumba cha 11, kilichopo  juu, mwisho kabisa mwa jengo la minara ya PPF lililopo kwenye makutano ya Ohio/Garden Avenue, katikati ya jiji la Dar es Salaam ndiyo iliyosababisha moto asubuhi ya leo majira ya saa moja u nusu hivi, na kusababisha jengo hilo ushika moto.

Imetaarifiwa kuwa walinzi  wa  jengo hilo  walishuhudia moshi mzito  ukitoka ndani ya  jengo hilo la ghorofa, ndipo walipotoa taarifa kwa vikosi vya zima-moto.

Kikosi cha uokozi kilifika kwa wakati katika eneo husika na pamoja na kuweko nyenzo katika jengo hilo za kukwea hadi orofa ya kumi na moja, ufupi wa mipira ya zima-moto ili kufikisha maji kwenye chumba kinachowaka moto ulikwamisha jitihada za kuuzima moto huo. Hata na hivyo, juhudi zilizofanywa na kikosi hicho zimefanikiwa kuuzima moto huo kuzima kabisa mnamo mwendo wa saa tano kasoro za adhuhuri.

Polisi wapo katika eneo hilo ili kulinda mali zisiporwe au kuharibiwa na vibaka.

Hakuna madhara yoyote ya moja kwa moja kwa binadamu yaliyoripotiwa. Thamani ya hasara iliyosababishwa na moto huo nayo haijafahamika.
.

Utapeli: “Imenitokea kwa mara ya pili - Waelewe matapeli waliokubuhu Dar”

WAELEWE MATAPELI WALIOKUBUHU HAPA DAR ES SALAAM.
IMENITOKEA MM LEO 02/02/2013 KWA MARA YA PILI

Kuna utapeli fulani unaendelea Tanzania na inaelekea wanaoufanya wamefanikiwa sana na wanaendelea kufanikiwa kwani ni wa muda mrefu sasa.

Nadhani matapeli hawa wanatumia ujinga wetu maana sisi sio watu wakutafuta sana usahihi wa mambo kabla ya kusema au kutoa maamuzi, pamoja na ujinga wetu wa kutaka kufanikiwa kwa haraka kwa njia yeyote ile hata kama hatujafanya kazi na bila kutumia akili.

Utapeli huu sio mwingine bali ni ule wa wale watu wanaompigia mtu simu wakijifanya wanakujua kabisa na wanaweza hata kukupa some backgrounds zako za kazi, ajira au elimu na meninge hadi ukashawishika kuwa unayeongea naye ni mtu unayemfahamu/munayefahamiana na hivyo kutokua na hofu na uhalisia wa anachokuambia.

Baada ya hapo wanaanza kukushawishi juu ya kuwasaidia kupata madawa ya kuhifadhi nafaka kwa madai kuwa mawakala wao ambo wamekua wakizipata toka kwao wameanza kuleta uswahili hivyo kwa vile unayeongea naye ndio anahusika na suppy, basi ameona ni vema akutumie wewe “mpendwa anayekujua” ili angalau upate hiyo commission kubwa ambayo huwapa ho mawakala na mugawane kidogo. Mara nyingi wanasema wanafanya kazi na shirika la chakula duniani (FAO) au shirika la wakimbizi duniani (UNHCR) na wako Kigoma.

Zaidi ya mwaka mmoja sasa nikiwa ofisini walinipigia na aliyekua anaongea name alianza kwa kujitambulisha kama graduate wa kitivo cha uhandishi cha chuo Kikuu Mlimani na kwamba tulisoma wote mwaka mmoja wakati nikisoma degree ya kwanza lakini huenda simkumbuki kwa sababu nilikua kiongozi wa fellowship na siwezi kuwa nakumbuka wote niliokua nawaongoza. Yeye alikuWa fellowship.  Alikua akiongea kwa kicheko na “bwana yesu” asifiwe nyingi ili
kunionesha ni kwa kiasi gani namfahamu na tunafahamiana. Kwa bahati mbaya wakati ananipigia nilishasikia kwa umbali juu ya utapeli huo ambao kwa kipindi hicho ndio ulikua umeanza tu na kushika kasi huku watu wengi wakiwa wamepoteza mamilioni. Hivyo alipoanza kuongea ujinga wake wa kunipa commission and all that, nilimwambia tu kuwa sina muda wa kujihusisha na biashara aliyokua “anataka kunisaidia ili nipate pesa za bure”, kwa haraka na bila jasho. Alikua disappointed sana kwa jibu langu hasa kutokana na muda mrefu alioutumia kunishawishi nikubali “msaada aliokua ananipa kama mpendwa mwenzake”.
Leo asubuhi majira ya saa nne nilipokea simu kwenye line yangu ya tigo na number iliyonigia ni 0717-093260. Mtu aliyenipigia alikua anaongea kwa uchangamfu mkubwa na kwa furaha huku akitaja majina yangu yote na kuniuliza iwapo kwa sasa niko DSM au nimesafiri. Aliniambia kuwa kafurahi kusikia kuwa niko DSM kwani ndipo zilipo ofisi zao na kwamba alitaka kuniunganisha zao ili nikachukue mzigo ambao utakua na cha juu kizuri sana. Nilipoona anaendelea nilimuomba ajitambulishe.... akaniambia anaitwa Lameck na kuwa alishafanya kazi Planet International hapa chuo kikuu. Alipotamka hivyo nikaanza kupata ukakasi kwani hapajawahi kuwa ofisi ya kampuni hiyo hapa Mlimani. Nikamuuliza yuko wapi kwa sasa na kwa msisitizo akanijibu kuwa kwa sasa yuko Serengeti National Park.

Nikamuuliza iwapo anafanya kazi na TANAPA... akasema hapana bali yuko na shirika moja la Kijerumani  linalojishughulisha na wanyamapori... na akijua kuwa niko Chuo Kikuu alitafuta style nzuri ya “kuniingiza alipokusudia” ...maana alianza kunieleza kuwa shirika lao linafanya “tafiti za wanyama pori katika mbuga yetu ya Taifa kubwa sana”. Bado nikiwa najaribu kuunganisha “idadi ya nukta kadhaa” akaniona mjinga sana na kuanza kunielezea jinsi wanyawa walioko Serengeti wanavyo migrate kila mwaka kwenda Kenya... na kuwa wanahama wengi kama elfu mbili hivi... (nikapata nukta nyingine)... then nikaingilia na kumsaidia kuwa hawavuki kwa maelefu bali ni zaidi ya milioni moja wanahama na kurudi kila mwaka. Pomaja na utafiti kazi nyingine wanayofanya ni pamoja na kutoa chanjo kwa wanyama hawa maana wanaporudi wanakua wamerudi na magonjwa toka Kenya.

Hapa ndipo alipopotea njia zaidi kwani kati ya jambo ninalolijua kwa mapana kidogo ni hii movement ya wild beasts, zebra na wengine walioko Serengeti . Nikamuonesha kushangaa kuwa wanawezaje kuwapa chanjo  wanyama wengi namna hii (na kumuonesha najua chanjo ni nini nikajifanya mhaya kidogo na kutamka vaccination)... akaanza kujichanganya kuwa wao wana njia tatu za kutoa chanjo maana ni kweli kuwa wanyama ni wengi... kwanza wanatengeneza majosho/mabwawa/madimbwi ambayo wanaweka dawa na hiyo wale wanyama wanapokua wanarudi wanatumbukia na hivyo automatically wanakua wamepata chanjo. Hapa akachemka zaidi...nikamuuliza hivi kuogesha ng’ombe kwenye majosho ni chanjo au ni kuua kupe na viroboto? Nikamuuliza kuna chanjo inafanyika juu ya ngozi?... alipoona hana majibu akauma maneno mawili-matatu halafu akasema njia ya pili wanayotumia ni kuwakamata wale wakubwa kama tembo na wengine na kuwapiga sindano za chanjo.... nikajizuia kucheka. Alipoona swali lingine linafuata kabla hajaanza kuningiza kwenye “undani/details za deal” lenye commission ...akaomba udhuru kidogo kuwa bosi wao kaingia ofisini mara moja na hivyo atanipigia baadaye kidogo...akakata simu na ukawa ndio mwisho wa mawasiliano

Alipokata simu tu nikam-text kuwa angeendelea tu na ujinga wake maana nawafahamu vema na wanachokifanya... na huo ukawa ndio mwisho wa ile namba kupatikana hewani baada tu ya ujumbe wangu kuwa delivered.

Ushauri Kidogo:

 • Unapojikuta kwenye mazingira ya mtu kujitambulisha kwako kwa nguvu kubwa huku ukiwa humfahamu, mpe nafasi ya kuongea
 • Unapojikuta kwenye mazingira ya kudanganyika kuwa unaweza kunufaika na kupa utajiri kirahisi kwa mtindo wa ki_DECI_DECI au kimuujizaujiza, usichanganyikiwe na kuanza kuutazama huo muujiza kama ndio umeshakufikia. Utafanya la muhimu sana iwapo utaruhusu akili yako kufanya kazi na kutafakari vema kila unachokiona au kukisikia
 • Kama unaweza, ni vema kurecord mazungumzo ambayo una wasiwasi nayo
 • Kama unaweza, una nafasi, na una matumaini kuwa polisi wanaweza kuwa na msaada kwenye hili, basi wasikilize watu hawa na kutafuta msaada wa polisi kwani utaokoa na wengine wasidanganyike
 • Tambua tu kuwa watu hawa wana mtandao mkubwa sana na mara nyingi wanafanya mambo yao wakiwa na taarifa za kuwatosha na wamejipanga. Unaweza ukawa kwenye mstari mwembamba sana unaotofautisha ukweli na uongo
 • Kwa nini bado makampuni ya simu yanaruhusu simu kutumika ikiwa haijasajiliwa? Na kama imesajiliwa, je wale wanaoandikisha hizi simu, wana ujuzi wowote wa kugundua kitambulisho halali na ambacho ni fake watu wanavyovitumia kusajilia simu zao?

Ufahamu na Akili tuliyonayo ukitumika vema bil haraka ya mafanikio tunaweza kukabiliana na changamoto nyingi za kitapeli tunazokumbana nazo!