Sunday, August 4, 2013

Kwa muda mrefu sasa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimekuwa kikitoa madai mazito dhidi ya CCM kutumia kikundi cha ulinzi na usalama kiitwacho Green Guard, kufanya vitendo vya siasa chafu, ikiwemo wizi wa kura, kupiga wapinzani wao (hususan CHADEMA), kufanya fujo kwenye mikutano ya hadhara, kuteka, kutesa na hata kuua wafuasi, wapenzi, mashabiki, wanachama na viongozi wa CHADEMA, katika maeneo mbalimbali nchini.

Katika tuhuma hizo, CHADEMA mara kadhaa, kimewahi kutoa ushahidi na kusema kiko tayari kuutoa ushahidi zaidi sehemu salama kwamba; vyombo vya dola vimekuwa vikihusika kutoa mafunzo ya kijeshi kwa Green Guard, kwenye makambi ya CCM kwa nia ya kudhuru wapinzani, walengwa wakuu wakiwa ni CHADEMA!

Hapa chini ni ushahidi mwingine. Utaona katika cheti hiki, wahitimu walipewa somo la 'mahusiano ya Green Guard na vyombo vya dola'. Mahusiano yapi? Hilo somo lilitolewa na nani? 

Aidha, katika ushahidi huu, ambao ni mwendelezo wa ushahidi kibao (wanaosubiri polisi na msajili wa vyama kuchukua hatua?), utaona Mkuu wa Wilaya, ambaye kinadharia anadhaniwa kuwa kiongozi wa serikali, (kivitendo sivyo, hovyo kabisa), ndiye mlezi wa makambi ya vijana wa CCM ambao wanafundishwa mbinu mbalimbali, ikiwemo kutumia silaha na kuua.

Kwa hii katiba mbovu ya sasa tuliyonayo (shukrani kwa CHADEMA kuwa custodian wa mchakato unaoendelea wa kuandika katiba mpya), DC ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, wakuu wa vyombo vya dola katika eneo au wilaya husika, wakati mwingine (au mwingi?) wanafanya kazi kwa maelekezo yake na kuripoti kwake.

Kama ilivyosemwa hapo awali, huu ni mwendelezo wa ushahidi. Kuna vyeti vimeshawekwa hapa, kuna kitabu kiliwekwa hapa, kuna picha kibao zimewekwa hapa; hadi sasa ushahidi wote ni undisputable kuwa CCM wanafundisha vijana wao mbinu za kijsehi, kwa ajili ya kuwashambulia wapinzani. Kile kitabu chao kimeeleza hivyo ukurasa wa 87.

Punde ushahidi wa mitaala inayotumika kufundisha makambi ya vijana wa CCM, mbinu za kuteka, kutesa na kuua, itawekwa hadharani. 

Mathalani, kule Ulemo, Singida wakati wa uchaguzi wa Igunga, walifundishwa hata namna ya kuchoma sindano za virusi vya UKIMWI!

Pia ushahidi zaidi wa namna serikali inavyotumika ku-patron haya masuala ambayo yamechangia sana kuharibu mahusiano ya kisiasa, kijamii na kiuchumi katika nchi hii.

Kwa leo, tujadili haya....wakati tunajadili, tumuulize Amiri Jeshi Mkuu, mbona amekaa kimya kauli ya Dkt. Slaa, aliyomtaka awaambie Watanzania ile bunduki aina ya bastola, yenye uwezo wa kubeba risasi 8, namba J137, kutoka CHINA, iliingiaje nchini bila kibali, kisha ikatumika kufundisha vijana wa CCM kwenye makambi yao! Huu ni mfano mmoja tu.

Tangu kutolewa kwa kauli hiyo, mwaka jana, si Amiri Jeshi Mkuu, wala vyombo vya dola, vilivyotoa ufafanuzi wa jambo hilo la hatari. Silaha isiyokuwa na kibali, kuwa mikononi mwa vijana wa CCM. Makambini!

Wakati akina Hammy-D & co, wanakuja kila siku na maneno ya kutunga, wakirudia hoja zile zile za uongo na propaganda kwa kubadili maneno na herufi, watu wanaotaka mabadiliko na kuitakia mema nchi hii, kwa kuhakikisha CCMM inaondolewa madarakani, tuendelee kuzungumza ukweli wenye hoja zilizojaa facts kama namna hii;


0 comments:

Post a Comment