Thursday, August 8, 2013

Natoa taarifa hii ili mwanachama yeyote wa CUF (MWANAUME AU MWANAMKE) mwaminifu, anayefahamika vizuri ndani ya chama au katika tawi lake, mwenye elimu ya kuanzia kidato cha nne kwenda juu na mwenye uwezo mkubwa wa kujitolea (Kwa sababu majukumu ya utendaji wa chama si ajira) aombe kutumikia nafasi hii.

Katibu wa Naibu Katibu Mkuu Bara niliyefanya naye kazi kwa miaka miwili Ndugu. Venance Chalamila, amechaguliwa kuwa Katibu mtendaji wa taasisi ya vijana iitwayo YALD hivyo anapumzika majukumu ya Ukatibu wa Naibu Katibu Mkuu Bara wiki kadhaa kutoka sasa.
...
Ukiona unaweza, tuma CV yako kwenye;
cuftanzania@yahoo.com

au tuma nyaraka zilizo katika "hard copy" kwa;
KATIBU MKUU,
THE CIVIC UNITED FRONT CUF,
S.L.P 10979,
DAR ES SALAAM.

au ziwasilishe nyaraka zako OFISI KUU YA CUF DAR ES SALAAM iliyoko karibu na Buguruni Sokoni.

Mwisho wa kuleta nyaraka hizi kwa njia nilizozitaja ni ijumaa 16 Agosti 2013 saa 8 Mchana.

Ninaweza kufanya kazi na mwanachama yeyote atakayekuwa na uwezo.

Namtakia kila le heri ndugu. Venance na namtaka aendeleze juhudi za kufanya kazi kwa bidii huko anakokwenda, aliitumikia nafasi hii kwa weledi mkubwa na Abarikiwe sana.

J. Mtatiro,
Naibu Katibu Mkuu,
The Civic United Front - CUF(Tanzania Bara),
+255717536759.

0 comments:

Post a Comment