Thursday, July 25, 2013

Kuna taarifa ambazo si vyema zikaendelea kuenea kwa namna inavyotaarifiwa.

MWENYEKITI wa Taifa, Freeman Mbowe leo alifika Makao Makuu ya Polisi leo mchana kama alivyokuwa ametakiwa kwa ajili ya mahojiano.

Itakumbukwa awali alitakiwa afike hapo Julai 23, 2013 mchana, lakini baadae, kutokana na sababu ambazo zilikuwa hazizuiliki, zikihusisha masuala ya kisheria, alitakiwa kufika siku inayofuata, yaani leo Jumatano, Julai 24, 2013, mchana.

Katika mahojiano ya leo, polisi wameendelea kumtaka Mwenyekiti Mbowe awapatie ushahidi walionao CHADEMA, juu ya tukio la bomu lililorushwa kwenye mkutano wa hadhara wa chama hicho, viwanja vya AIC, Soweto, Arusha.

Mwenyekiti Mbowe ameendelea kusimamia maamuzi ya Kamati Kuu ya CHADEMA iliyoazimia kuitaka serikali kuunda Tume (huru) ya Kimahakama kuchunguza tukio hilo na ushahidi utatolewa mbele ya tume hiyo.

Baada ya mahojiano na polisi, huku Mwenyekiti aliondoka. Hayuko chini ya ulinzi wowote, wala mahala popote. Wakili wake ataweka msimamo huo wa mteja wake katika maandishi na kuwasilisha polisi.

Vinginevyo "ulinzi" unaoweza kuwepo sasa hivi ni majukumu, kwa maana ya kutingwa na shughuli za kusonga mbele kwenye mapambano haya, hasa wakati huu ambapo chama kinamalizia kuimarisha mkakati wa kukishusha chini kwa wanachama kupitia kanda na kusimamia dhana ya "CHADEMA ni msingi", mambo ambayo yameshaanza kung'oa mizizi ya CCM iliyokuwa imesalia na kutishia kabisa uhai wa chama hicho kilichopoteza ushawishi wa kisiasa, kiuchumi na kijamii miongoni mwa Watanzania wanaochemka joto la mabadiliko ya utawala na mfumo.

Makamanda watulie. Wasimame imara. Wasiyumbishwe.

Asanteni

Makene
0752 691569/0688 595831

0 comments:

Post a Comment