Friday, June 21, 2013

Zipo taarifa kuwa kuanzia mwezi Julai mwaka huu, gharama za bima ya gari zitaogezeka.

Mathalani, gari ambalo lilikuwa likilipiwa shilingi 60,000/= sasa litalipiwa shilingi 250,000/= hivi.

Mchangiaji mmoja amesaidia kutoa ufafanuzi kuhusu hilo kwa kusema, "Haihusu comprehensive ni kwa 3rd party tu na sababu kubwa ya kuongeza ni kwa sababu gharama za garages zimekuwa kubwa na fraud zimekuwa nyingi sana kwenye motor."

Hata hivyo, mchangia mada mwingine alipinga ufafanuzi huo kwa kusema, "frauds ziko kwenye comprehensive, na ukiongelea gharama za garage ni comprehensive pia."

Napo ufafanuzi zaidi ukatolewa ya kuwa, "Ukigonga wewe wakati una 3rd party, bima yako inatengeneza gari la yule uliyemgonga na malipo mengine kwa yule uliyemgonga. Sasa wao wa kampuni za bima wanasema hivi, kwenye biashara ya bima kipengele cha motor kila mwaka kinapata hasara kwa kuwa gharama za garage ni kubwa na pia kuna fraud. Ili kupunguza hasara ni bora wapandishe 3rd party ambayo ni compulsory kuliko comprehensive ambayo ni ya hiari. Baada ya kusema hayo kama unaona 3rd part imekua ghali kata comprehensive."

Basi, hebu tusubiri ufafanuzi zaidi kutoka kwa mamlaka husika.

0 comments:

Post a Comment