Friday, March 29, 2013

KUZALIWA;
Mhe. Salimu Hemed Khamis(Marehemu) alizaliwa shehia ya Mizingani jimbo la Chambani tarehe 20 Septemba 1951 .

ELIMU YA MSINGI;
• Mwaka 1959-1960 alisoma katika shule ya msingi Pandani.
• Mwaka 1960 – 1967 alisoma katika shule ya msingi Kengeja na kuhitimu elimu ya msingi.

ELIMU YA SEKONDARI;
• Marehemu alijiunga na masomo ya sekondari mwaka 1968 katika shule ya Sekondari ya Chambani iliyoko Pemba na alisoma hapo hadi mwaka 1969.
• Ilipotimu mwaka 1970 marehemu aliendelea na masomo ya sekondari katika shule ya sekondari ya Fidel Castro na alihitimu mwaka 1971.
• Mwaka 1972 marehemu alijiunga Lumumba Sekondari, zamani ikiitwa “LUMUMBA COLLEGE” kwa ajili ya masomo ya kidato cha tano sita na alihitimu mwaka 1973.

ELIMU YA JUU;
• Marehemu alisomea shahada ya kwanza Bachelor of Science in Agronomy 1978 -1982 huko Havanna nchini Cuba.
• Mwaka 1988 – 1989 alijiunga na chuo cha Commonwealth Mycological Institute kilichoko nchini Uingereza (UK) na kusomea shahada ya uzamili ya masuala ya “Plant Disease Management” yaani “utaalamu wa magonjwa ya mimea”

MAFUNZO YA KITAALAMU;
• Mwaka 1987 - Marehemu alishiriki na kuhitimu mafunzo ya uongozi ya “SENIOR MANAGEMENT COURSE ON AGRICULTURE” huko nchini Uswisi.
• Mwaka 1989 - Marehemu alishiriki mafunzo maalum ya “UTAFITI WA VIRUTUBISHI WA MIMEA” yaani “IDENTIFICATION OF PATHOGENIC FUNGI AND BACTERIA” katika chuo cha “Commonwealth Mycological Institute” CMI huko LONDON - Uingereza,

UTUMISHI WA UMMA;
Marehemu ametoa mchango mkubwa katika sekta ya umma kwa upande wa Zanzibar na Tanzania Bara kutoka na elimu kubwa na adimu aliyojaliwa na mwenyezi mungu sambamba na ujuzi;
• Marehemu alikuwa mwalimu wa Shule ya Sekondari Mtambile Pemba chini ya wizara ya elimu mwaka 1974 – 1978.
• Mwaka 1977 – 1978 alifundisha pia katika Shule ya Sekondari Fidel Castro – Pemba.

Katika kusukuma gurudumu la kilimo ambalo ndilo uti wa mgongo wa taifa, marehemu alitumia ipasavyo utaalam na ujuzi wake wa hali ya juu wa masuala ya usimamizi wa mimea kwa kusimamia mashamba kadhaa ya kilimo;
• Mwaka 1984 - 1996 alikuwa meneja wa shamba la Shirika la Sukari na Manukato la Mahonda lililoko Zanzibar.
• Mwaka 1997 hadi 2001 marehemu alikuwa meneja wa shamba la Kampuni ya SAS rasmi likijulikana kama SAS Company Ltd lililokuwa mkoani Morogoro.

KUJIUNGA NA SIASA NA KUWA MBUNGE.
• Marehemu alijiunga na The Civic United Front - CUF Chama Cha Wananchi kama mwanachama hai mwaka 1997 na alikitumikia chama kwa uaminifu na jitihada kubwa.
• Mwaka 2005 marehemu Salim Hemed Khamis alipitishwa na Chama Cha Wananchi CUF kuwa mgombea ubunge katika jimbo la Chambani na alishinda uchaguzi wa Oktoba 2005 na kuwa mbunge halali wa jimbo hilo.
• Mwaka 2010 alipitishwa tena chama ili akiwakilishe katika kinyang’anyiro cha ubunge katika jimbo hilohilo na alishinda tena na kuongoza kipindi cha pili hadi umauti ulipomkuta.
• Alikuwa Waziri Kivuli wa Wizara ya Kilimo,Chakula na Ushirika tangu Mwaka 2005 hadi 2010 Bunge la Tisa lilipo maliza muda wake

NAFASI ZA UONGOZI NDANI YA CHAMA;
Kutokana na uwezo wake mkubwa katika masuala ya uongozi, chama kilimpatia marehemu Salim Hemed Khamis dhamana kubwa za uongozi;
• Mjumbe wa Kamati ya Utendaji na Mjumbe wa Mkutano mkuu wa tawi la Kimbuni tangu mwaka 1997 hadi anafariki.
• Mjumbe wa Kamati ya Utendaji jimbo la chambani na Mjumbe Kamati ya Utendaji ya Wilaya ya mkoani Pemba tangu mwaka 2005 hadi anafariki.
• Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya CUF taifa mwaka 2011 – 2012.
• Marehemu alikuwa mjumbe wa mkutano mkuu wa Taifa 2005 hadi anafariki na mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa - CUF tangu mwaka 2011 hadi 2012.
• Marehemu alikuwa Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi kwa ngazi ya taifa mwaka 2011 na kwa namna ambavyo alithamini masuala ya uongozi, ilipofika mwaka 2012 aliomba kupumzika wadhifa wa Ukurugenzi wa kitaifa ili aelekeza nguvu zaidi jimboni jambo ambalo liliridhiwa na chama.

Hadi anafariki marehemu ameacha vizuka wawili na watoto wanane.


"CHAMA CHA WANANCHI CUF KIMEPOTEZA NGUZO MUHIMU, TUNAWASHUKURU WATANZANIA WOTE WANAONDELEA KUTUMA SALAMU ZA POLE KWA VIONGOZI WA CHAMA NA WAFIWA".
SOURCE: Julius S. Mtatiro

0 comments:

Post a Comment