Saturday, March 16, 2013

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya CFAO Motors Roddy Sharp (kulia) akiongozana na Waziri wa Nchi Mh. Anne Ruth Herkes wa Wizara ya Uchumi na Teknolojia ya Ujerumani (kushoto) baada ya kuupokea Ujumbe kutoka nchini Ujerumani kunakotengenezwa magari aina ya Volks Wagon walipofika kushuhudia uzinduzi wa showroom mpya ya Kampuni ya Alliance Autos wauzaji wa magari ya Volkswagon. Kushoto ni Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Mh. Klaus Peter Brandes aliyeambata na ugeni huo.
Waziri wa Nchi Mh. Anne Ruth Herkes wa Wizara ya Uchumi na Teknolojia ya Ujerumani akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika hafla ya uzinduzi wa Showroom mpya ya magari ya Volkswagon ya Kampuni ya Alliance Autos iliyopo Pugu/Nyerere road jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Msaidizi wa Mkurugenzi wa CFAO Motors Mama Maria Petro akipokea wageni waalikwa.
Mgeni rasmi Waziri wa Uchukuzi Mh. Dkt Harrison Mwakyembe akizungumza na wageni waalikwa pamoja na ujumbe wa wafanya biashara kutoka Ujerumani walioongozwa Balozi wa Ujerumani nchini Klaus –Peter Brandes katika hafla ya kuzindua Showroom ya magari ya kampuni ya Alliance Autos inayouza magari aina ya Volkswagon ambapo pamoja na mambo mengine amepongeza hatua hiyo na kusema serikali iko bega kwa bega na wafanya biashara wabunifu na pia kuuhakikishia ujumbe kutoka Ujerumani kuwa serikali imeweka mazingira bora ya kuwekeza hivyo wasisite kujitokeza.
Mkurugenzi wa Biashara wa CFAO Motors Wayne Mcintosh (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya CFAO Motors Roddy Sharp(kulia) wakifurahia hotuba ya Dkt. Mwakyembe.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya CFAO Motors Roddy Sharp akizungumza wakati wa uzinduzi huo ambapo amesema kufuatia kupanuka kwa kampuni ya Alliance Autos na kuongezeka kwa wateja tumeonelea ni vizuri kufungua showroom mpya ya magari ya Volkswagon ambapo wateja wanaweza kuitembelea wakati wowote.
Mgeni rasmi Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe (wa pili kulia) akifurahia jambo wakati Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya CFAO Motors Roddy Sharp (hayupo pichani) akisoma hotuba yake kwenye hafla ya uzinduzi wa Showroom mpya ya magari aina ya Volkswagon ya Kampuni ya Alliance Autos (T) LTD. Kulia ni Waziri wa Nchi Mh. Anne Ruth Herkes wa Wizara ya Uchumi na Teknolojia wa Ujerumani. Kushoto ni Tender Manager wa CFAO Motors Bw. Marco Kahabi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Ujerumani, Prof. Harald Braun (wa pili kushoto).
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Ujerumani, Prof. Harald Braun akizungumza machache na wageni waalikwa ambapo amesema ziara ya Ujumbe kutoka Ujerumani imekuwa na mafanikio si tu kwa mazungumzo na Serikali bali kwa kufanikiwa kuhudhuria ufunguzi wa Showroom mpya ya magari ya Volkswagon ya kampuni ya Alliance Autos na kupata fursa ya kubadilishana mawazo na wafanyabiashara watanzania.
Bw. Lionel Roux wa CFAO Paris Ufaransa akitoa salamu kwa wageni waalikwa wakati wa ufunguzi wa Showroom mpya ya magari aina ya Volkswagon ya Kampuni ya Alliance Autos.
Meneja Mkuu wa Alliance Autos, wakala wa Volkswagen nchini, Alfred Minja (kushoto), Afisa Mauzo wa Kampuni ya Alliance Autos (T) LTD Bw. Julius Guni (katikati) na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya CFAO Motors Roddy Sharp wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Ujerumani, Prof. Harald Braun(hayupo pichani).
Johns Wiseman wa Volkswagon Group katika uzinduzi huo.
Tender Manager wa CFAO Motors Bw. Marco Kahabi (kulia) akiteta jambo na Mgeni rasmi Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harrison Makyembe. Wa pili kulia ni Balozi wa Ujerumani nchini Mh.Klaus Peter Brandes.
Afisa Mauzo wa kampuni ya Alliance Autors Julius Guni akizungumza na vyombo vya habari akisema kuwa kampuni hiyo imeweza kutambulisha magari mapya aina ya Volkswagon amboyo yamefanyiwa ‘engineering’ ya Kijerumani hivyo ni magari madhubuti sana.
Aidha amesema kupitia Chama cha Wauza Magari (TMTA) tunaitaka serikali kuhakikisha inaangalia sana suala la ushuru ili kila mtu aweze kuwa na uwezo wa kumiliki gari, hivyo tukishirikiana na makampuni mengine yanayouza magari kupambana tuweze kupata unafuu.
Afisa Mauzo wa Kampuni ya Alliance Autos (T) LTD Bw. Julius Guni na mmoja wa wageni waalikwa wakikagua magari mapya aina ya Volkswagon ya Kampuni ya Alliance Autos kwenye showroom mpya iliyozinduliwa jana jijini Dar na Waziri wa Uchukuzi Dr. Mwakyembe.
Mkurugenzi Mshirika wa IMMMA Advocates Lawrence Masha akipata maelezo ya gari aina ya Volkswagon TIGUAN kutoka kwa Afisa Mauzo wa Kampuni ya Alliance Autos (T) LTD Bw. Julius Guni wakati wa hafla ya uzinduzi wa showroom hiyo.
Meneja Mkuu wa Alliance Autos, wakala wa Volkswagen nchini, Alfred Minja (kulia) na Afisa Mauzo wa Kampuni ya Alliance Autos (T) LTD Bw. Julius Guni (katikati) wakibadilishana mawazo na mmoja wa wageni waalikwa wakati wa uzinduzi huo.
Picha juu na chini ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya CFAO Motors Roddy Sharp akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa showroom mpya ya magari aina ya Volkswagon ya Kampuni ya Alliance Autos jijini Dar.
Baadhi ya wageni waalikwa wakinywa na kufurahi baada wakati wa uzinduzi wa Show room mpya ya Kampuni ya magari aina ya Volkswagon ya Alliance Autos jijini Dar.
Meneja Masoko wa CFAO Motors Tharaia Ahmed (kulia) akibadilishana mawazo na mmoja wa wateja waliohudhuria uzinduzi huo.
Picha juu na chini ni Wakwetu Band ikiongozwa na Carola Kinasha kutoa burudani kwa wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa showroom mpya na ya kisasa ya magari aina ya Volkswagon ya Kampuni ya Alliance Autos.
Uzinduzi huo ulihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Ujerumani na Ujumbe wake.
Afisa Mauzo wa Alliance Autos David Kritsos (katikati) na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi huo.
Operations Manager wa Golden Tulip Bw. Aatish Ladwa(kushoto) na mmoja wa wageni waalikwa.
Warembo wa Volkswagon waliokuwa wakikaribisha wageni kwenye hafla ya uzinduzi wa showroom mpya ya Kampuni ya Alliance Autos iliyopo maeneo ya Pugu/Nyerere road jijini Dar es Salaam.

0 comments:

Post a Comment