Saturday, March 30, 2013

Joseph J.Mungai MB (mstf)
P.O.BOX 34 Mafinga
S: 0753 192999
BP: 
jjmungai@tatepa.com

BARUA YA WAZI KWA TUME YA ELIMU YA KUFELI 60% MTIHANI WA KVI 12012 ILIYOTEULIWA NA MHE WAZIRI MKUU
29/03/2013
Kumb Na. JJM/2013/ELIMU/19

Kwa Mwenyekiti
Tume ya Elimu  ya Kufeli KIV
Ofisi ya Waziri Mkuu

DAR ES SALAAM

Ndugu Mwenyekiti

KUONGEZEKA WANAOFELI KIV KUTOKA 9.7% MWKA 2007 HADI 60% 2012

1.1   Nnawapongeza kwa kuteuliwa na ahsante kutupa fursa wadau fwa elimu kuwaletea maoni na  au/ushauri.

2.0  Mimi ni mdau wa elimu, niliyewahi kuwa Mwenyekiti mwanzilishi wa Mufindi Education Trust (MET) iliyoanzisha katika wilaya ya Mufindi na kuziendesha  kwa mika zaidi ya 10 Sekondari  9 za: (1) JJ Mungai (2) Sadani (3) Itengule  (4) Igowole (5) Itandula (6) Mgololo (7) Kibengu ( 8) Mdabulo na ( 9) Nyololo; ambazo sasa ni za serikali. Aidha nimewahi kuwa waziri wa Elimu na Utamaduni  mwaka 2000 hadi 2005.

3.0 Kabla ya kutoa ushauri naoba kuipa Tume yako ufahamu  wa ukweli ufuatao:

3.1 Kufeli mwaka 2012 kidato cha Nne (KIV) kwa asilimia 60 halikuwa tukio lililoibuka ghafla bali waliofeli (Divisio 0) mtihani huo waliongezeka kutoka mwaka 2007:9.7% ; 2008:16.3%; 2009:27.5%; 2010:49.6%; 2011:46.4% na sasa 2012:60%!!!!!

3.2 Kabla ya hapo waliofeli kidato cha Nne (KIV) WALIPUNGUA kutoak mawka 1998:24:3%:; 1999:20.0% 2000:21.6% 2001:22.6%, 2002:12.7%; 2003:12.2%, 2004:8.7%, 2005:10.7%, 2006:10.9%, na 2007:9.7% wastani wa kufeli 2004 hadi 2007 ni 10%. Tazama hotuba ya bajeti ya Waziri wa Elimu na Utamaduni ya mwaka 2005/2006 kielelezo Na. 75.4 ukurasa wa 100; na BEST (Basic Statics in Education, National Data) ya miaka  husika.

3.3 Kati ya 2004 na 2007 waliofeli kidato cha Nne  walikuwa wastani wa 10% ambayo   inavumilika. Kwa nini kati ya 2007 na 2008 kulikuwa na mruko kutoka 9.7% hadi 16.3%? Huo ukawa ndio mwanzo wa kuonge zeka  kila mwaka hadi kufikia 60%  ya mwaka huu!!!!! Wizara ya Elimu na OWM-TAMISEMI baada   ya  matokeo mabaya ya mwaka 2010 walifanya  “utafiti kudadisi sababu   za ufaulu huo mbaya” na taarifa yake ipo kwenye maktaba a Wizara” na iliandaliwa kauli ya waziri isomwe Bungeni”, lakini  hadi leo haikusomwa.   Ukweli ulifichwa; na mficha ugonjwa kifo kitamuumbua. Nukuu zangu kutoka Taarifa moja     isiyo   ya siri ya ndani    ya wizara ya Elimu.

4.0 Kwa maoni yangu maboresho ya Elimu ya Serikali ya Awamu ya Tatu ambayo  yanaweza kusomwa katika maandiko   mawili ya Wizara ya Elimu yaitwayo: (a) Nyaraka za Elimu 1999 hadi 2005, na ( b) Sheria ndogo za Elimu au kanuni za Elimu zilizotungwa kuyapa maboresho  hayo uzito wa kisheria yamepelekwa NYARAKA ZA KALE (ACHIVES) kabla  ya wakati wake. Maboresho yamewekwa kando moja     baada ya jingine  au hayakusimamiwa ipasavyo na Elimu yetu imerudi  ilivyokuwa kabla  ya mwaka 2000.

USHAURI:

5.0 Kwa kuwa Elimu ni nyenzo muhimu   sana kuliko zote katika kuboresha nguvu kazi ya Taifa na kucho cchea  maendeleo  ya nchi nimeamua kutonyamaza na kuwa muwazi kabisa, ingawaje mimi ni mwanasiasa  niliyestaafu. Kwa hiyo NASHAURI mambo yafuatayo:

5.1 Utaratibu  sahihi wa kupanda madarasa kwa ufaulu ( achievement based progression)  uliowekwa na waraka wa Elimu Na. 1& 2 wa 2002 urejeshwe na uimarishwe   bila  kuchelewa kuasnzia Darasa la kwanza,  la pili na la Tatu ambayo      Mwalimu Mkuu siku zote anayo madaraka    ya kukalilisha, kama mwanafunzi   hajazijua “K” 3: kusoma, kuandika na kuhesabu.

5.2 Tume ya Mhe. Waziri Mkuu ifanye kwanza REJEA ya maandiko ya Wizara ya Elimu  niliyoyataja akatika 4(a) na (b) hapo  juu yaliyomo maboresho ya elimu ya 2002-2005 yaliyofanikisha kufaulu vizuri  katika   Elimu ya Msingi na Sekondari miaka ya 2004-2007; badala ya kutumia muda mwingi na fedha n=yingi kugundua upya gurudumu.

5.3 Taasisi  ya Elimu Tanzania ( Tanzania  Institute of   Education –TIE) iagizwe na iachiwe  kutekeleza wajibu  wake wa kisheria chini ya Sheria ya Elimu ya 1995 wa kuandaa na kuboresha mitala.

5.4 Wanasiasa tuache kuamua bila  kuzingatia ipasavyo utafiti na ushauri wa kitaaluma kuhusu Elimu ya Taifa letu.

Kutokana  na uamuzi mbaya na kuchelewa kuchukua  hatua ya marekebisho kila inapobidi; Elimu yetu imerudi ilikokuwa  kabla ya mwaka 2000. Rika zima la kielimu limepotea!!!sasa tunavuna kilichopandwa vibaya. Kwa hiyo TUJISAHIHISHE kwa kuacha kuingilia na kuamua bila kuzingatia  utafiti na ushauri fwa kitaaluma ili tusije kuumbuliwa tena na matokeo mabaya kama    hayo ya kidato cha Nne   ya mwaka 2012. Aidha inafaa matokeo ya mitihani yawe yanatangazwa kwa uwazi hata kama ni mabaya kwa sababu, narudia “anayeficha maradhi  kifo kitamuumbua.”

Wasalamu

Joseph J Mungai MB mstf
MDAU WA ELIMU

---
Shukurani ya nakala: FrancisGodwin blog

0 comments:

Post a Comment