Friday, March 22, 2013

Mwanafunzi mmoja wa kidato cha Nne katika shule ya kutwa ya Sekondari Mataka, wilayani Tunduru huko Ruvuma, Mussa Habibu amenusurika kifo baada ya kupigwa na walimu saba kwa tuhuma za kumtongoza mwalimu wake.

Mtuhumiwa alipohojiwa akiwa hospitalini, alijitetea kuwa si yeye aliyetamka maneno hayo bali ni pacha wake.

Inaelezwa kuwa mwanafunzi na mwalimu huyo walikutana katika nyumba moja walimojihifadhi kukwepa mvua.
00:00
00:00
Yaliyotukia - WAPO FM Radio
00:00
00:00
Taarifa - TBC1
00:00
00:00
00:00
Taarifa - Radio One Stereo
Hayati Mwl Nyerere anaendelea kuelezea kuhusu Watanganyika kujitawala na mipango ya ujenzi wa vijijii.
00:00
00:00
Wosia wa Baba - Julius K. Nyerere
Suala la Lwakatare: Wanasheria CHADEMA wazungumza

Kiongozi wa jopo la wanasheria watano wanaomtetea Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA, Wilfred Lwakatare, Wakili Tundu Lissu, akiwawakilisha wenzake, ameongea na vyombo vya Habari akiwa Makao Makuu ya CHADEMA na kuzungumzia masuala kadhaa kutokana na sakata hili.

Lengo kuu la mkutano huo na wanahabari lilikuwa ni kuutarifu umma wa Watanzania kupitia kwa wanahabari juu ya hatua ambayo mawakili hao wameamua kuchukua kwa kupeleka ombi Mahakama Kuu ya Tanzania, chini ya hati ya dharura ili Mahakama hiyo ya juu iitishe mafaili yote mawili yaliyofunguliwa kuhusu kesi ya Lwakatare, yaani faili la kesi iliyofutwa na faili lililofunguliwa baada ya kesi ya awali kufutwa, wakiiomba mahakama iangalie na kujiridhisha.

Kupitia hati hiyo ya dharura, mawakili hao wanaiomba Mahakama Kuu:

- Ifute hati ya DPP iliyotolewa jana ikifuta mashtaka ya awali
- Ifute amri ya mahakama ya iliyotolewa kumaliza kesi iliyofunguliwa awali kabla ya kufutwa jana
- Ielekeze Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, itoe maamuzi kama ilivyokuwa imepanga kutoa kabla 'haijaingiliwa' kwa DPP kuifuta kesi mahakamani.
- Na pia wameiomba Mahakama Kuu, itamke kuwa hicho walichofanya waliomfungulia kesi Lwakatare ni matumizi mabaya ya; 1. Mamlaka ya DPP, 2. Mfumo wa Mahakama na 3. Kuingilia uhuru wa Mahakama.

Mbali ya maelezo hayo, Wakili Lissu pia amejibu maswali ya wanahabari, ambapo walitaka kujua masuala mbalimbali kuhusu kesi na mashitaka yanayomkabili Lwakatare, akisema:

Mosi, Ili kosa liwe la kigaidi, ni lazima kuwepo maelezo yanayofafanua kuwa kuwa mtuhumiwa alikuwa na malengo au nia ya kigaidi; lakini hakuna maelezo ya namna hiyo kwenye hatia ya mashtaka kueleza ‘terrorism intention’. Alifafanua kuwa kwa maoni yake, Lwakatare amefunguliwa mashtaka ya kigaidi kwa nia tu ya kutaka asote gerezani, kwa sababu waliofungua mashtaka wametaka hivyo… ateseke!

Pili, Nolle prosequi iliyowasilishwa jana na DPP kufuta kesi iliyofunguliwa Jumatatu Machi 18, 2013 kwa ridhaa yake inazua maswali sana (questionable) sana kwasababu hakuna mahali mazingira yanaonesha iliwasilishwa kukidhi masuala mawili muhimu, maslahi ya umma na kuboresha utendekaji wa haki.

Endelea kusoma habari hii kwenye FikraPevu.com

0 comments:

Post a Comment