Saturday, January 19, 2013

Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Azania wakiwa wamejipanga kumpokea mgeni rasmi katika mahafali ya kidato cha Sita ya shule hiyo Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa yaliyofanyika leo jijini Dar.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akibadilishana mawazo na baadhi ya Wanafunzi wa shule ya Sekondari Azania ambapo na yeye pia alikuwa ni miongoni mwa baadhi ya viongozi waliosoma shule hapo baada ya kuwasili kwenye hafla mahafali ya wanafunzi wa kidato cha sita.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akipunga mkono kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Azania waliojipanga mstari kumlaki kwa furaha huku akiwa ameambatana na Mkuu wa Shule hiyo Bw. Bernard Ngoze na Makamu Mkuu wa Shule hiyo Bi. Elizabeth Ngoda (kulia).
Mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa akisaini daftari la wageni la Shule ya Sekindari Azania katika sherehe za mahafali ya Kidato cha sita shuleni hapo.
Mkuu wa shule ya Sekondari Azania Bw. Bernard Ngoze akizungumza na mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa na kumwelezea changamoto mbali mbali zinazoikabili shule hiyo. Wa kwanza kulia ni Makamu Mkuu wa Shule hiyo Bi. Elizabeth Ngoda na Makamu wa pili shuleni hapo Mwl. Joram Nkya.
Kutoka kushoto ni Mgeni maalum aliyewahi kusoma shuleni hapo Bw. Ali Said Mwema, Mjumbe wa Bodi ya Shule hiyo Bi. Hilda Luhanga na Msaidizi wa Meya Jerry Silaa Bw. Anthony William wakimsikiliza mkuu wa shule ya sekondari Azania (hayupo pichani) wakati akiongea na Mgeni rasmi.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa akiongozwa na Makamu Mkuu wa Shule ya Azania Bi. Elizabeth Ngoda kutazama baadhi ya picha zinazoonyesha hali ya utunzaji wa mazingira tangu awali mpaka sasa ambapo kwa kiasi kikubwa shule hiyo imeweza kuboresha na kutoa elimu ya mazingira kwa wanafunzi wa shule hiyo. Mstahiki Meya amepongeza juhudi zao na kuwataka shule nyingi za jijini zilizochini ya manispaa ya Ilala kuiga mfano wa shule ya Azania katika kutunza Mazingira.
Baadhi ya picha zikionyesha harakati za utunzaji wa Mazingira wa Shule ya Azania unaosimamiwa na Mkuu wa Shule hiyo Bw. Bernard Ngoze ambaye naye alikuwa miongoni mwa wanafunzi waliosoma shule hiyo.
Vijana wa Skauti wa shule ya Sekondari Azania wakitoa heshima kwa mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa alipowasili eneo maalum palipofanyika sherehe za mahafali ya kidato cha Sita.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akisalimiana na kuwapongeza baadhi ya wanafunzi wa kidato cha Sita wa Shule ya Sekondari Azania.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akipokea heshima kutoka kwa vijana wa skauti wa shule hiyo.
Kiongozi wa gwaride la skauti la Azania akisalimiana na mgeni rasmi Meya Jerry Silaa.
Baadhi ya Wanafunzi wa kidato cha sita wa shule ya Azania wakiimba wimbo wa Taifa baada ya mgeni kuwasili.
Skauti wa shule ya Azania wakuupa heshima wimbo wa Taifa.
Meza kuu ikiimbia wimbo wa taifa.
Baadhi ya Wazazi na walezi waliohudhuria hafla ya watoto wao.
Vijana wa Skauti wakionyesha manjonjo yao mbele ya mgeni rasmi kwenye mahafali hayo.
Binti Pekee wa kikundi cha Skauti cha Azania sekondari aliyeshangaza wengi kwa kutembea na kamba huku akijiamini vilivyo wakati wa sherehe za mahafali hayo.

0 comments:

Post a Comment