Friday, January 25, 2013


  >>> ILIKUWA YAA MWISHO KIMKOA, HATA MWAKA 2011
  >>> HAIKUTOA MWANAFUNZI WA KIPAJI HATA MMOJA
  >>>  ILITIA DOA KWA UDANGANYIFU ( SHULE YA MSINGI MAKUNDA ILIFUTIWA MATOKEO, shule hii alisoma Mhe. MWIGULU )

Nikiwa kama mtaalamu katika maswala ya elimu ninaamini:
   1. Nina mchango wa masuala ya elimu
   2. Kuainisha tatizo kitaalamu
   3. Kweli ninajua kero za wilaya ya IRAMBA
Leo nitajikita kwenye elimu kwasababu ni ufungua wa maisha, ukikosa elimu hasa dunia ya sasa utakuwa mvamiaji kwavile hauna funguo. Kwahali hiyo wan-Iramba hatuna ufunguo wa maisha, kama tunao ni mbovu hauwezi kufungua maisha. Bila shaka tutakuwa kwenye dunia nyingine ya wasiokuwa kwenye maisha. Binafsi sipendi hali hii, inanikera sana tena sana tu. Ninalazimishwa tu kusikia hali mbaya ya elimu.
    Malengo ya taathimini hii :
   1. Kuonesha hali halisi ya elimu IRAMBA
   2. Kuwarahisishia wapenda maendeleo waone pa kuanzia
   3. Kuonesha jinsi nilivyoguswa na kuwagusisha wana-Iramba
   4. Wenye majigambo kuhusu Iramba hasa wana-siasa wangu kuwaambia waache porojo kuna kazi.
   5. Kuwatangazia wana-iramba hili ni janga la kimkoa
   6. Kuomba pole binafsi kwa jinsi nilivyoumizwa na matokeo haya, nazani mnajua maumivu ya mapenzi, mi naipenda Iramba.
 Ngoja nianze kutiririka tathimini yangu:
Iramba ni wilaya yenye majimbo mawili ( Iramba Magharibi la Mhe. Mwigulu Nchemba na Iramba Mashariki la Mhe. Salome Mwambu ).  Iramba ina wabunge wawili, na madiw zaidi ya 35 ukiacha watendaji wengine.
   Iramba ina shule za msingi 169, shule zilizofanya mtihani 163. Iramba imeonesha kumiliki hati ya kuwa ya mwisho, mwaka 2012 imekuwa ya mwisho kimkoa na hata miaka mitatu ya nyuma iliyopita vilevile. Uzito wa swala hili ni mkubwa sana. Shule zina wanafunzi 84,000 hii ni idadi kubwa hivyo athari zake ni kubwa sana hasa miaka ijayo.
     Msimamo wa matokeo kufanya vizuri kimkoa:
         1. Manispaa Singida
         2. Singida vijijini
         3. Manyoni
         4. Iramba
Wanafunzi walifanya masomo matano, jumla ya alama zote ilikuwa ni 250. Iramba ilipunguziwa alama 180 kati ya 250 ili apatikana mwanafunzi wa kwenda vipaji maalumu lakini hakuapatikana. Ilipochagua wanafunzi kwa ala juu ya 100 kati ya 250 shule nyingi zilikosa wanafunzi. Wanafunzi walichukuliwa mpaka alama 70 ambazo ni sawa na alama 14 kwa somo. Hizi alama ni chini ya nusu za alama za somo.
      Nitataja shule na nafasi zao kiwilaya kwenye mabano, hizi ni baadhi tu : Iguguno (27), Sophia (23), Mwandu (19), Kinyangiri ( 25), Lyelembo ( 26 ), Lukomo (38), Kitumbili ( 80 ), Tumuli ( 76),Yulansoni ( 91), Ishenga (104 ), Nkenke (115), Milade ( 139 ), Nyeri (147 ) Hizo nfasi ni kati ya shule 163 zilizofanya mtihani.
 Iramba ina walimu 1442, kati ya hao walimu 1349 ndio wanaofundisha. Ukichukua hesabu ya wanafunzi 84,000 ugawe kwa mkondo wa wanafunzi 40 utapata madarasa 2100, kama kila dara litahitaji mwalimu mmoja basi kuna uhaba wa walimu kama idadi ya waliopo. Mwaka jana Iramba ilipata walimu 173, hii ni idadi ndogo sana kwa hitaji tena wengine hawakuj kuripoti.
Kuna changamoto nyingi zinazopelekea matokeo mabaya ; ulevi, uhaba wa nyumba, uhaba w walimu, wanafunzi waliofaulu na kutokwenda shule za sekondari, utoro, ubovu wa miundo mbinu shuleni, na zingine nyingi tu.
Changamoto zingine ni madarasa la kwanza na la pili kufundishwa na walimu wasio wazoefu, na walimu hao kutopewa muda wa kupumzika kw kuondoka mapema kwa maandalizi zaidi. Pia kutopewa motisha kutokana na ugumu wa kazi yao. Wanafunzi wakiiva madarasa ya chini mzigo unakuwa mdogo madarasa ya juu.
    Tutegemee nini kwa matokeo ya darasa la saba 2013 ? Hapatakuwa na mabadiliko, Iramba itakuwa ya mwisho tena. Dawa ya kubadili mojawapo ni wazazi kushirikiana na wazazi kikamilifu na kuacha dhana ya shule ni mali ya serikali. Mwanfunzi anaishi sehemu mbili ( Shule na Nyumbani ), Shule anakaa kwenye mawe, nyumbani anakaa kwenye sofa. Wazzi wanapaswa kuachana na ubinafsi. Familia nyingi hazina vitabu hata nakala moja tu. Wanasiasa wanawalemaza kwa kuahidi hewa kuwafanyia mambo mazuri.
   Hawa darasa la saba waliofaulu wengi wao mwisho ni KIDATO CHA PILI, safari yao itaishia hapo. Jamii inapaswa kujipanga upya. Wakiachia waendelea KIDATO CHA NNE wataangukia tumbo.
Naomba kuwasilisha hoja
Ayoub Idd
Mwana-mikakati imara
simu 0713 610893
e-mail: ayoubimangi@yahoo.com

0 comments:

Post a Comment