Friday, December 7, 2012

72' GOAL!! Sentongo anashinda goli lake la pili la mchezo.
51' GOOAL! Robert Sentongo anamalizia mpira mzuri ulipigwa na Hamis Kiiza.
11' GOOAL!! Okwi anapiga shuti kali sana.

  • Kikosi Cha Uganda: Hamza Muwonge, Dennis Iguma, Godfrey Walusimbi, Isaac Isinde, Henry Kalungi, Geoffrey Kizito, Moses Oloya, Hassan Wasswa, Joseph Ochaya, Robert Sentongo, Emmanuel Okwi
  • Kikosi Cha Tanzania: Juma Kaseja, Erasto Edward Nyoni, Maftah Amir Mrisho, Shomari, Kapombe, Kevin Yodan, Amri Kiemba, Salum Abubakar, Damayo Raymond, Mwinyi, Kazimoto, Mrisho Alfan Ngasa, John Raphael Bocco
Picture
Abdallah Juma akishangilia kwa kuonyesha maandishi kwenye fulana yake baada ya kufunga penalti ya mwisho usiku huu
Na Mahmoud Zubeiry, Kampala via blog

ZANZIBAR imekufa kiume, baada ya kutolewa kwa penalti 4-2 na Kenya katika Robo Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole mjini hapa, kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika ya 120.

Hadi mapumziko, timu hizo zilikuwa zimefungana bao 1-1, Zanzibar wakitangulia kupata bao dakika ya 20, mfungaji Khamis Mcha ‘Vialli’, aliyeunganisha pasi ya Jaku Juma, baada ya kazi nzuri ya Suleiman Kassim ‘Selembe’.

Kenya ilisawazisha dakika ya 29, mfungaji Mike Barasa ambaye alifumua shuti lililowachanganya Nahodha, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na kipa wake, Mwadini Ally na kutinga nyavuni.

Zanzibar waliuanza vizuri mchezo huo na kusukuma mashambulizi mfululizo langoni mwa Kenya kutokea pembeni, ambao walionekana kabisa kuzidiwa na kutumia muda mwingi kucheza kwa kujihami.

Hata hivyo, baada ya kupata bao la kusawazisha, kibao kiliwageukia Wazanzibar na kuanzia hapo Kenya ndio waliokuwa wakisukuma mashambulizi mfululizo langoni mwa wapinzani wao.

Kipindi cha pili, mchezo ulianza kwa kasi na Zanzibar walionekana kucheza kwa tahadhari wakiwadhibiti Wakenya, huku wakiendelea kumiliki zaidi mpira.

Hali hiyo ilizaa matunda ya Heroes kupata penalti dakika ya 75 baada ya mshambuliaji Juma Jaku kuangushwa kwenye eneo la hatari, Joackins Atudo, wakati anakwenda kumuona kipa Duncan Ochieng na refa Thierry Nkurunzinza wa Burundi akaamuru pigo hilo.

Nahodha Aggrey Morris alikwenda kupiga penalti hiyo na kuikwamihsa kimiani kuipatia bao la pili Zanzibar.
Hata hivyo, bao hilo halikudumu sana, kwani dakika ya 80 Kenya walisawazisha kupitia kwa Mike Barasa tena, akiunganisha krosi ya Paul Were aliyeingia kuchukua nafasi ya Ramadhan Mohamed dakika ya 46.   

Hadi dakika 90, timu hizo zilikuwa zimefungana 2-2 na mchezo ukahamia kwenye dakika 30 za nyongeza, ambako Kenya walishinda.

Khamis Mcha ‘Vialli’ alikosa penalti ya kwanza kabisa na Issa Othamn Ally akakosa ya pili, wakati Aggrey Morris na Samir Hajji Nuhu walifunga. Kwa upande wa Kenya, waliofunga ni Mike Barasa, Joackins Atudo, Edwin Lavatsa na Abdallah Juma aliyepiga ya mwisho.

Kwa ushindi huo, Kenya itacheza Fainali na mshindi wa mechi ya pili kati ya Uganda na Tanzania, wakati Zanzibar itawania nafasi ya tatu dhidi ya timu itakayofungwa usiku huu.

Kenya: Duncan Ochieng, Anthony ‘Modo’ Kimani, Joackins Otieno Atudo, David Owino Odhiambo, Abdallah Juma Baya, David Ochieng, Kevin Omondi Obwaka, Humphrey Ochieng Mieno, Clifton Miheso Ayisi/Paul Were Ooko, Ramadhan Mohamed Salim/Edwin Lavatsa Jumba na Mike Baraza.

Zanzibar: Mwadini Ally, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Nassor Masoud ‘Chollo’, Samir Hajji Nuhu, Aggrey Morris Ambroce, Sabri Ally Makame, Suleiman Kassim ‘Selembe’, Khamis Mcha ‘Vialli’, Jaku Juma Jaku/Abdallah Othman Ally, Amir Hamad Omar na Adeyom Saleh Hemed/Seif Rashid Abdallah.
Picture
Wachezaji wa Zanzibar Heroes na wa Kenya wakiwani mpira wakati wa mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya michuano ya Cecafa Challenge uliofanyika katika Uwanja wa Mandela Nambole Jijini Kampala. (picha: ShaffihDauda.com)

0 comments:

Post a Comment