Friday, November 30, 2012

Ndiyo wakuu ,heshima kwenu ! Hayawi hayawi yamekuwa , Leo kuanzia saa 2 usiku ,harakati za M4C homa na kiboko ya ccm pamoja na vibaraka wake itazinduliwa rasmi jijini mwanza kwa kanda ya ziwa katika hoteli ya Gold Crest live kupitia star television. Ni mara nyingine tena leo umma wa watanzania utashuhudia kama kweli bado kanda ya ziwa ni ngome ya ccm au la.

Leo kutwa nzima nimekuwa na mizunguko yangu hapa city center ambapo gumuzo kubwa ni harakati za mabadiliko i .e M4C ambayo itazinduliwa kesho na uongozi wa Kitaifa.


Pia katika mizunguko hiyo nimekutana na magari kadhaa yenye alama/ nembo M4C . Baba wa taifa la India , Mahatma Gandhi alipata kusema " Be part of the change you wish to see in this world." Kwa tafsiri isiyo rasmi, alisema "Kuwa sehemu ya mabadiliko uyatakayo kwenye ulimwengu huu."


Vilevile naomba ninukuu maneno ya lango la kuingia makaburi ya waislamu pale mtaa wa Langolango-mwanza yanayosema "Swali kabla ya kuswaliwa." Tuungane kwa unyonge na umaskini ili kuitafta Tanzania tuitakayo kwa ajili yetu ,watoto wetu na vizazi vijavyo . Naomba kuwasilisha.

0 comments:

Post a Comment