Friday, November 9, 2012

Picture
Eliakim Maswi

Tafadhali bofya kifute cha pleya hapo kumsikiliza Spika wa Bunge, Anne Makinda akisoma Bungeni leo, ripoti ya Kamati Ndogo ya Bunge iliyochunguza kashifa iliyomhusisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini na Nishati, Eliakim Maswi akiwatuhumu baadhi ya Wabunge kula rushwa kutoka kwenye makampunmi ya mafuta.

Baada ya kusoma ripoti, Spika alitoa uamuzi wake.

Ripoti hiyo ya Kamati ya Bunge iliyoongozwa na Mbunge wa (Mlalo-CCM), Brigedia Jenerali mstaafu Hassan Ngwilizi iliundwa Julai 2 mwaka huu na ilishakamilisha kazi yake na kuiwasilisha kwa Spika, Septemba 20, 2012.

Pamoja na Mwenyekiti Ngwilizi, wajumbe wengine wa kamati hiyo walikuwa Said Arfi (Mpanda Kati), John Chiligati (Manyoni Mashariki), Goesbert Blandes (Karagwe) na Mbunge wa Viti Maalumu, Riziki Omary Juma.

Ripoti ya Kamati ya Bunge - Spika, Anne Makinda

0 comments:

Post a Comment