Friday, November 2, 2012

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
                                                                                                 WIZARA YA MAMBO YA NDANI
                                                                                                    JESHI LA POLISI TANZANIA


Anuani ya Simu “MKUUPOLISI”
Ofisi ya  Inspekta  Jenerali wa Polisi,
Simu : (022) 2110734 
Makao Makuu ya Polisi,
Fax Na.(022)2135556 
S.L.P. 9141,
Unapojibu tafadhali taja:
DAR ES SALAAM.



02 Septemba 2012

                                                                            TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


                                MABADILIKO KWA BAADHI YA MAKAMANDA WA MIKOA NA VIKOSI.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IJP Said Mwema, amefanya mabadiliko kwa baadhi ya makamanda wa Polisi wa mikoa na vikosi.

Mabadiliko hayo ni pamoja na aliyekuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani SACP Ernest Mangu anayekwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza kuziba pengo la marehemu ACP Liberatus Barlow, ACP David Misime aliyekuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Temeke kwenda kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma kuchukua nafasi ya SACP Zelothe Steven anayestaafu. Vilevile, aliyekuwa kamanda wa Polisi Viwanja vya Ndege ACP Ulrich Matei anakwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani.

Aidha, wengine ni kutoka Makao Makuu ya Polisi na Makao Makuu Idara ya Upelelezi ambapo ACP Engelbert Kiondo kutoka makao makuu Idara ya Upelelezi  anakwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Temeke, ACP Rashid Seif kutoka Makao Makuu ya Polisi Kwenda kuwa Kamanda wa kikosi cha Tazara, ACP Deusdedit Kato kutoka Makao Makuu ya Polisi kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Viwanja vya Ndege, ACP Shaban Hiki kutoka Kamanda wa Kikosi cha Ufundi kwenda Makao Makuu ya Polisi na ACP Lucas Mkondya kutoka Makao Makuu ya Polisi kwenda kuwa Kamanda wa Kikosi cha Ufundi.

Mabadiliko hayo pia yamehusisha aliyekuwa Afisa Mnadhimu wa kikosi  cha Usalama Barabarani  ACP Johansen Kahatano anayekwenda kusimamia  Mradi wa SMARTER Traffic ambapo nafasi yake itachukuliwa na aliyekuwa RTO mkoa wa Pwani ACP Swalehe Mbaga. Uhamisho huo pia umewahusisha baadhi ya Wakuu wa Operesheni wa Mikoa, Wakuu wa Vikosi vya Kutuliza Ghasia vya Mikoa, Wakuu wa Polisi wa Wilaya na Wakuu wa Upelelezi wa Wilaya.

Uhamisho huo ni wa kawaida kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya Jeshi la Polisi.


Imetolewa na:
 Advera Senso-ASP
 Msemaji wa Jeshi la Polisi (T).

0 comments:

Post a Comment