Thursday, November 8, 2012

Hukumu ya aliyekuwa mbunge wa arusha Mh Godbless Lema itasomwa leo katika mahakamu kuu kanda ya arusha.Hukumu hiyo inafuatia baada ya mbunge huyo kukata rufaa baada ya kuvuliwa ubunge wa arusha mjini baada ya wanachama watatu wa chama cha mapinduzi CCM kufungua kesi ya kupinga ubunge wake wakitoa sabubu ya kuvunjwa kwa baadhi ya sheria za uchaguzi wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 mkoani arusha ambapo mbunge huyo alikuwa anapambana vikali na mh Batilda Burian ambaye kwa sasa ni balozi wa Tanzania nchini Kenya.


Moja ya taswira za aliyekuwa mbunge wa arusha Mh Godbless Lema
Hapa lema akipambana na polisi akiwa sambamba na mbunge wa arumeru mashariki Mh Joshua Nassari

0 comments:

Post a Comment