Thursday, November 15, 2012

Msanii wa muziki kwa jina, “Diamond Platnumz” kupitia  tovuti yake anaelezea mkasa wa ajali iliyompata hivi majuzi:

Tarehe 10 ya mwezi wa 11 siku ya juma mosi ni moja ya siku ambazo sitozisahau maishani mwangu.

Baada ya kumaliza majukumu yangu ya kila siku, nilikwenda masaki kumwona mmoja wa jamaa zangu wa karibu nikiwa na Blogger wangu Bestizzo pamoja na mwanafamilkia ya wasafi Dumi (Dancer).

Mishale ya saa moja hivi nikiwa maeneo ya masaki karibu na kona ya msasani nilipata ajali ambayo haikuwa kubwa sana ingawa imesababisha uharibifu kwa kiasi kikubwa.

Kama mjuavyo barabara ya Msasani ni ndogo na gari huwa haziko katika mwendo wa kasi... ghafla dereva wa pikipiki alikatisha mbele yangu na katika kujaribu kumkwepa nikagonga gari ndogo aina ya Rav4 ambapo ilisababisha dereva wa pikipiki kuanguka katikati ya gari zote mbili.

Hiyo ndio hali halisi ya ajali niliyokutana nayo Jumamosi iliyopita.

Namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kutunusuru wote bila majeraha makubwa zaidi ya maumivu tu ya hapa na pale.

0 comments:

Post a Comment