Sunday, October 21, 2012


Shyrose Banji mjumbe wa mkutano mkuu umoja wa wanawake Tanzania ambaye pia ni mbunge katika bunge la Afrika Mashariki amenusurika kufukuzwa kwenye mkutano wa kumchagua mwenyekiti mpya wa umoja huo baada ya kumwuliza swali gumu Sofia Simba kama ifuatavyo:
"Wewe ukiwa mwenyekiti wa UWT kwa kipindi cha miaka minne iliyopita hatujawahi kukuona ukisimama jukwaani kutetea Chama."

Wafuasi wa Simba walilipuka kama gas iliyoshika moto kwa kutaka atolewe nje ya ukumbi.
Mwenyekiti wa uchaguzi Profesa Tibaijuka alitumia mamlaka yake kumlinda Shyrose Bhanji asitolewe njie kwa vile ni haki yake kumwuliza swali mgombea.

Jibu la Sofia Simba kwa swali la Shyrose lilikuwa jepesi kama ifuatavyo:
"Inaonekana aliyeuliza swali hajakomaa katika siasa za nchi, ndio maana ameambulia kuzomewa na wajumbe wa mkutano huu. Habwatuki bungeni au majukwaani kwa vile yeye ni serikali, na hata mbunge wa CCM hapaswi kukikosoa chama chake. Mimi si mithili ya upinzania kukaa na kukiosoa chama napaswa kukitetea. Anayesema Sofia Simba hajafanya kitu anajidanganya kwani wapiga kura wako kwenye matawi, kata, wilaya na mikoa, hao ndio wapiga kura wa chama na mimi kama mwenyekiti wa UWT nilijiimarisha katika ngazi za chini."

Maoni ya mwananchi (
Nguruvi3 )
Shyrose nadhani ''she is in wrong place at wrong time'
Swali lake ni la msingi kabisa kwasababu alitaka kujua nini Sophia Simba amekifanya kutaka nafasi tena.

Swali hili halikulenga kumuumiza Sophia pengine lingemjenga sana. Kama kuna alichokifanya huu ndio ulikuwa wasaa wa yeye kuueleza mkutano mkuu kwa ufasaha. Nafasi hiyo adhimu akaitumia kutuonyesha aina ya viongozi tulio nao.


Mwenyekiti wa UWT ni mjumbe wa vikao muhimu vinavyotoa maamuzi ya nchi.

Jibu la kuwa yeye amejiimarisha katika matawi na hicho ndicho alichokifanya kwa umma wa wanawake wa Tanzania.
Kwanini tusiendelee kuwa masikini, tuzizongwe na ujinga na maradhi?

Tunatakiwa tufanye maamuzi yenye busara na hekima 2015. Kinyume chake tutaendelea kushudia uzezeta ukiwa ni sehemu ya tamaduni zetu.

0 comments:

Post a Comment