Tuesday, October 2, 2012

Ndugu Amani Mgheni amemtahadharisha Rais Kikwete kuwa asipokuwa makini katika kusimamia matumizi sahihi ya rasilimali za Taifa ataandika historia ya kuwa rais wa kwanza kushtakiwa mahakamani kwa kushindwa kusimamia rasilimali hizo.

Mgheni ambaye ni Katibu wa Jimbo la Segerea wa CHADEMA, alitoa tahadhari hiyo wakati akitoa salamu kwenye mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika katika mtaa wa Ugombolwa, Kata ya Segerea, jijini Dar es Salaam.

Alisema kuwa kama Rais Kikwete asipowachukulia hatua za kisheria kwa kuwafikisha mahakamani watendaji wanaotuhumiwa kutumia vibaya rasilimali za umma, chama chake kikiingia madarakani atahakikisha anashtakiwa. “Haiwezekani rasilimali za umma zinatumiwa vibaya, kama vile wanyama kutoroshwa kwenda nje ya nchi, lakini watuhumiwa wanaachwa tu bila kuchukuliwa hatau za kisheria,” alisisitiza Mgheni na kuongeza: “Kama rais  asipowachukulia hatau za kisheria, maana yake ni kwamba  anajua kilichokuwa kinaendelea, hivyo kwa kuwa yeye ndiye aliyewateua, basi, 2015 ataweka historia ya kuwa rais wa kwanza kusimama kizimbani kujibu tuhuma za kushindwa kusimamia vizuri rasilimali za umma.”.

Endelea kusoma habari hii ya James Magai kwenye gazeti la Mwananchi

0 comments:

Post a Comment