Friday, October 19, 2012

Mwanafunzi  wa Kidato cha Kwanza  katika Shue ya Secondari ya Chamriho iliyoko wilayani Bunda mkoani Mara amefariki dunia baada ya kupigwa na radi huku wenzake watatu wakinusurika.

Radi hiyo pia imeiteketeza kwa moyo nyumba walimokuwemo vijana hao.

Tukio hilo ambalo limeleta maafa  na kuacha makubwa, limetokea katika kijiji cha Nyang’aranga katika kata ya Mugeta  majira ya saa tatu usiku wakati marehemu na wenzake walipokuwa wakijisomea ndani ya nyumba hiyo.

Afisa mtendaji wa kijiji hicho, Fikiri Magunila  amemtaja  mwanafunzi aliyepigwa na radi kuwa ni Karosi Joram aliyekuwa akisoma  kidato cha kwanza katika Shule hiyo.

Kumekuwepo na matukio ya radi kali katika kijiji hicho ambapo miaka ya hivi karibuni radi iliua watu wawili.

---
Habari hii imeandikwa na Pascal  Buyaga - Bunda, Mara.
Imewasilishwa na Magiri Paul wa wotepamoja.com

0 comments:

Post a Comment