Thursday, October 18, 2012

Picture
Mwenyekiti mpya wa CCM mkoa wa Singida Mgana Izumbe Msindai akitoa shukurani zake kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi (hawapo kwenye picha) kwa kumpa kura za kutosha.Kulia ni mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone.
KILIMANJARO, Moshi Vijijini: 
via MichuziJr blog

Mbunge wa Moshi Vijijini Dkt. Cyril August Chami ameshinda uchaguzi wa CCM na kuwa Mjumbe wa NEC kupitia Wilaya ya Moshi Vijijini kwa kupata kura 967 (96%) kati ya kura 1008 zilizopigwa.

Vile vile, ndugu Gabriel Masenga ametetea kiti chake cha Uenyekiti wa CCM, Wilaya ya Moshi Vijijini.

SINGIDA 
via Nathaniel Limu, DewjiBlog Team, Singida)

Mkutano Mkuu wa uchaguzi CCM mkoa wa Singida umemchagua Mgana Izumbe Msindai kuwa mwenyekiti wake kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Msindai maarufu kwa jina la CRDB benki, ameshinda kiti hicho baada ya kupata kura 673 dhidi ya 41 za mpinzani wake Amari Rai.

Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Joramu Allute, alipata kura 194 kwenye duru ya kwanza. Baada ya kupata kura ambazo hazikutosha mzee Allute aliondoka wakati mkutano huo ukiendelea.  Katika kura hizo zilizopigwa awali, Msindai aliongoza kwa kupata kura 407 na Amani Rai kuambulia 238.

Zoezi hilo lilirudiwa kwa kile kilichodaiwa kuwa hakuna mgombea aliyepata nusu ya kura za wajumbe kama inavyoainishwa kwenye katiba ya CCM.

Rai baada ya kubaini kuwa sio rahisi kumbwaga Msindai, aliomba kujitoa na kwamba kura alizopata, apewe Msindai kwa madai anamheshimu sana.

Hata hivyo, msimamizi wa uchaguzi huo makamu mwenyekiti wa pili CCM Tanzania bara John Chiligati, alitupilia mbali ombo la Rai kwa madai kwamba katiba ya CCM hairuhusu mgombea kujitoa katika hatua iliyofikiwa.

Kura ziliporudiwa mara ya pili, kama ilivyotarajiwa, Msindai aliibuka na ushindi.

Katika hatua nyingine, msimamizi wa uchaguzi huo Chiligati,aliwatangaza washindi wawili kutoka kila wilaya kuwa wajumbe wa halmashauri kuu mkoa ambao ni Duda Juma Mughenyi na Sara Abel Mkumbo kutoka manispaa ya Singida.

Alitaja wengine kuwa ni Manase Sabasaba na Abdala Ghamayu kutoka Singida vijijini, Chambo Yahaya na Omari Mohammede(Ikungi), Hamisi Kinota na Lyanga Timoth (Iramba), Rehema Cizuma na Amosi Budodi (Manyoni) na kutoka wilaya mpya ya Mkalamani William Nyalandu na Mlingi Salima Selemani.

0 comments:

Post a Comment