Tuesday, August 28, 2012


MrokiM blog -- Mtu mmoja anadaiwa kufa kwa kupigwa risasi kichwani huku wengine kadhaa wakijeruhiwa vibaya kwa Risasi za moto baada ya Polisi kuwarushia Risaasi za moto na mabomu ya machozi waandamanaji wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mjini Morogoro.

Polisi waliwatawanyisha wanafuasi hao walipokuwa wakifanya maandamano maeneo ya Msamvu mjini Morogoro mchana wa leo. Polisi walitibua maandamano hayo waliyodai hayakuwa rasmi, kwa kutumia mabomu ya machozi.

--- ENDS ---

Lukwangule blog -- POLISI Mkoani Morogoro wameingia kwenye  marumbano na Chadema baada ya  kutokea kwa mauaji ya kijana Ally Shana Zone   wakati wa maandamano ya CHADEMA mkoani hapa.

Kifo hicho kilichotokea majira ya mchana kimedaiwa kusababishwa na risasi na Polisi wakati wa purukushani za kuzima maandamano ya Chama hicho leo.

Pia imedaiwa katika purukushani hizo, Frank Valimba na Hashimu Seif walijeruhiwa sehemu mbalimbali za miili yao.

Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Slaa, alisema katika mkutano wa hadhara eneo la Uwanja wa Ndege Mjini hapa  kuwa amewateua viongozi wanne wakiongozwa na Mbunge Tundu Lissu, pamoja na Mwanasheria, Amani Mwaipaja kukutana na Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Faustine Shilongile kuangalia kwa undani mazingira ya kifo cha kijana huyo.

Chadema baada ya kuzungunza na  Viongozi wa Polisi, wamekubaliana Mwili wa kijana huyo uhifadhiwe chumba cha Maiti cha Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro ili kupicha uchunguzi wa kitaalamu kubaini chanzo cha kifo hicho.

Kwa mujibu wa Tundu Lissu, Uongozi wa Polisi umeamua kupata Daktari aliyetajwa kwa jina moja la Dkt. Mataka ili kuenndesha uchunguzi huo ambapo Mwanasheria wa CHADEMA-Morogoro, Amani Mwaipaja atasimamia shughuli hiyo.

Lissu aliwataka wanachama wa Mkoa wa Morogoro walioshuhudia kijana huyo akipigwa mabomu ama risari wanatakiwa kujitokeza kutoa ushuhuda wakati wa uchunguzi wa kimahakama ili kudhibitisha kifo hicho kuwa ni cha mkono wa mtu.

Picture
Askari wa Kikosi cha kuzuia fujo FFU wakitoa onyo kwa waandamanaji kutawanyika (picha via Habari Mseto blog)
Picture
picha via WanaBidii google forums
Picture
picha via WanaBidii google forums
Picture
picha via WanaBidii google forums
Picture
Huyu ni Ally Zona muuza magazeti wa Msamvu Morogoro akiwa hajitambui baada ya kutandikwa risasi na Polisi kuzuia maandamano ya CHADEMA (picha Father Kidevu blog)
Picture
Huyu ni mwananchi aliyeuawa na polisi kufuatia maandamano ya amani ya CHADEMA leo asubuhi... Alikuwa ni muuza magazeti ambaye hakujihusisha hata na maandamano. Wengine watatu wamejeruhiwa kwa risasi. (picha: CHADEMA Blog)
Picture
Ndugu wa marehemu Ally Nzona akiwa amesimama kando ya mwili wa ndugu yake katika hospitali ya Mkoa wa Morogoro, ambaye alifariki kwa kupigwa risasi na polisi wakati wa maandamano ya amani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mjini Morogoro (picha via Habari Mseto Blog)
Picture
Kijana Hashimu Seif aliyepigwa risasi mguuni akiwa hospitali.
Picture
Kijana Frank Valimba akionyesha majeraha aliyoyapata tumboni kutokana na vurugu hizo.
Picture
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willibrod Slaa, akiwahutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Morogoro na vitongoji vyake, katika mkutano wa hadhara wa operesheni sangara, kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Uwanja wa Ndege (picha : Habari Mseto blog)
Picture
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lisu akizungumza na wananchi wa Manispaa ya Morogoro waliojitokeza katika mkutano huo. (picha Juma Mtanda blog)
Picture
Makamanda wa chadema wakiwa kwenye dk 1 ya maombolezo kwa kumkumbuka kijana Alli aliyepigwa risasi na polisi leo Morogoro. (picha: Hosea D. Mtui's facebook wall)
Picture
Mbunge wa viti Maalum CHADEMA Suzan Mungi akimwaga sera za chama hicho. (picha : Juma Mtanda blog)
Picture
Makamu Mwenyekiti CHADEMA Zanzibar Said Issa Mohamed akifafanua jambo kwa wananchi hao. (picha : Juma Mtanda)
Picture
Aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Igunda kupitia CHADEMA, Joseph Kashinde akizungumza na wananchi waliohudhuria katika mkutano huo (picha : Juma Mtanda blog)
Picture
Mbunge wa jimbo la Ubungo Jijini Dar es Salaam John Mnyika akipanda jukwaani wakati akiwasili katika uwanja wa shule ya msingi Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro. (picha: Juma Mtanda blog)
Picture
(picha: Hosea D. Mtui's facebook wall)
Picture
Baadhi ya wafuasi na wanachama wa Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA mkoani Morogoro wakiongozwa na polisi baada ya kuwatawanyisha walipokuwa wakifanya maandamano maeneo ya Msamvu mjini Morogoro mchana wa leo. Polisi walitibua maandamano hayo yanayodaiwa kutokua rasmi kwa mabomu ya machozi. (picha Father Kidevu blog)
Picture
(picha: Hosea D. Mtui's facebook wall)
Picture
Mkuu wa Operesheni Sangara-Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) BENSON KIGAIYA akiwa chini ya ulinzi wa Polisi wa FFU watano huku wengine wakinyatia kwa pembeni, akiambulia makofi ya mgongo na makalio. (picha: Juma Mtanda blog)
Picture
Mkuu wa Operesheni Sangara-Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) BENSON KIGAIYA akiwa chini ya ulinzi wa gari la polisi mara baada ya kukamatwa wakati wa zoezi la kuwapokea viongozi wa juu wa chama hicho kushindikana katika eneo la Msamvu kwa ajili ya maandamano kuelekea kwenye mkutano wa hadhara wa CHADEMA shule ya msingi Uwanja wa Ndege mkoani Morogoro. (picha : Juma Mtanda)
Picture
Huyu alikuwa akitembea huku gari la FFU likiwa nyuma yake baada ya kupigwa kwa mabomu eneo hilo la Msamvu. (picha : Juma Mtanda)

Msimamo wa JOHN MNYIKA kuhusu vurugu, risasi, kujeruhi na “kuua” Morogoro!

Niliwahi kutahadharisha baada ya tukio la Dkt Stephen Ulimboka kuwa serikali imeanza kutumia mbinu haramu kudhibiti fikra mbadala, CCM imeanza kuongoza serikali kiimla na ipo siku umma utafikia hatua ya kukiona kama chama cha mauaji.

Raia watatu wasio na hatia wamefyatuliwa risasi na mmoja amefariki. Haya yamefanyika kwenye maandamano ya amani ya wananchi kuwapokea viongozi wa CHADEMA kuelekea kwenye mkutano. Vurugu zimeanzishwa na polisi kwa mujibu wa mashuhuda wa ushahidi wa video.

Vyanzo vyangu vinaniambia sasa wameagiza gari tatu za FFU na gari za kuwasha toka Dar Es Salaam. Tuombe MUNGU wasiamue kuvuruga mkutano wa hadhara ambao wananchi wamekusanyika kwa wingi hivi sasa.

States captured by grand corruption of the ruling party cronies for so many years resorts to bullets as a way of stopping M4C through the ballot. Maisha ya wachache yako mashakani lakini si mabadiliko kwa maslahi ya wengi.

Source: wavuti

0 comments:

Post a Comment