Tuesday, August 28, 2012

Alifika nyumbani na kumlaghai mtoto Julius kwa pipi na kumuita uncle, uncle.

Akamvuta mpaka vichakani.

Akiwa tayari ameshashusha nguo, akataka kumlawiti.

Mtoto alipoona hivyo akaanza kupiga kelele na kupambana na mtuhumiwa.

Mtuhumiwa wa uasi alipoona mtoto anapiga kelele, akaanza kumshambuliwa kwa kumng'ata kwa meno mashavuni na kisha kumpiga na jiwe kwenye paji la uso.

Kwa bahati nzuri, mama aliyekuwa anashusha matofali jirani alisikia purukushani za kelele hizo kabla ya tendo baya la ulawiti kufanyika. Ndipo mama yule akawaita watu ambao walimkuta mtuhumiwa akiwa anaendelea na jaribio lake hilo la kulawiti.

Mtuhumiwa alifanikiwa kumwaga haja zake, ila hakufanikiwa kumuingilia mtoto kimwili, ndipo watu wenye hasira walipompa adhabu yake na yeye, kabla Polisi kufika na kumtia mbaroni.

Inasemekana kuwa mtuhumiwa huyu ndiyo tabia yake, mitaa ya Mbezi ya Kimara, amezunguka sana kuharibu watoto wa watu, ila hii ndio ilikuwa arobaini yake. Kila Nyumba akifika anauliza baba na mama wapo? akijibiwaa hawap,o anaanza shughuli zake.

Hivi sasa yuko mahututi katika Hospitali ya TUMBI, akingojea kusomewa mashtaka.
---

Picha na maelezo via  LadyJayDee blog 

0 comments:

Post a Comment