Friday, July 6, 2012


Joti.
Stori: Sifael Paul
BAADHI ya komediani wa kiume Bongo wamepigwa zengwe wakihusishwa na kuchochea vitendo haramu vya ushoga nchini, Amani linafunguka.
Gazeti hili lilielezwa kuwa kinachosababisha kuibuka kwa madai hayo ni kutokana na wanaume hao watafutaji kuingiza kama wanawake kwa kutupia mavazi ya kike na kujipodoa kuliko hata masistaduu wenyewe.
Kwa mujibu wa uchunguzi wa gazeti hili, makundi yanayotajwa kuangukia kwenye ishu hiyo ya kutoa hamasa ya ushoga ni Orijino Komedi ‘OK’ linaloruka hewani kupitia Runinga ya TBC1 na Ze Comedy wanaotamba kwenye Runinga ya EATV.
Katika uchunguzi huo, Lucas Mhuvile ‘Joti’ alishika namba moja kwa Kundi la Orijino Komedi akiongoza kwa kuigiza kama mwanamke huku akifuatiwa na Alex Chalamila ‘McRegan’, Isaya Mwakilasa ‘Wakuvwanga’, Emmanuel Mgaya ‘Masanja’ na Slivery Mujuni ‘Mpoki’.
Kwenye Kundi la Ze Comedy waliotajwa kuchochea ushoga kwa vijana wa Kitanzania ni Dickson Makwaya ‘Bambo’ na Masawe Mtata.
Gazeti hili lilipozungumza na baadhi ya wachekeshaji kuhusu wanaume kujigeuza wanawake badala ya kumtafuta mwanamke halisi kuigiza nafasi inayomhitaji mwanamke, walidai kuwa ni namna ya kujiajiri kuliko kuwa vibaka kwa kuwa soko la ajira ni tatizo Bongo.
Akizungumzia suala hilo, mmoja wa wabunge wa Zanzibar alisisitiza kuwa wasanii hao wanahamasisha ushoga hivyo wanapaswa kukemewa mara moja waache

0 comments:

Post a Comment