Wednesday, July 4, 2012

Wakati madaktari wakirejea kazini taratibu na kuhudumia Watanzania, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ilidaiwa jana kufukuza madaktari walio katika mafunzo kwa vitendo.

Msemaji wa madaktari hao, Frank Kagoro alidai jana kuwa madaktari hao walipewa barua za kufukuzwa, lakini walizikusanya na kuzirejesha kwa Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Alisema waliutaka uongozi wa Muhimbili kuzipeleka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kuwa wao wako chini ya Wizara.

Hata hivyo, Aligaesha alipohojiwa kuhusu kufukuzwa kwa madaktari hao, alisema hawezi kulizungumzia na kusisitiza kuwa halipo katika taarifa hiyo.

Wakati madaktari hao wakitaka Muhimbili iwarudishe serikalini, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imewaagiza madaktari hao waripoti wizarani kabla ya keshokutwa.

Msemaji wa Wizara hiyo, Nsachris Mwamwaja alisema madaktari hao wote nchi nzima, wanatakiwa kufika wizarani siku hiyo ili kuelezwa taratibu nyingine.

(habari via HabariLeo)

-----------------

Nakala ya agizo la taarifa kwenye barua hiyo inasomeka ifuatavyo:

TAARIFA KWA MADAKTARI WALIOPO KWENYE MAFUNZO YA VITENDO (INTERNS)WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII INAWATANGAZIA MADAKTARI WOTE WANAOFANYA MAFUNZO KWA VITENDO (INTERNS),  WALIOPEWA BARUA ZA KURUDISHWA  KWA KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII, WANATAKIWA KURIPOTI MAKAO MAKUU YA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII IFIKAPO SIKU YA IJUMAA TAREHE 6 JULAI, 2012.

IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI 
3/07/2012


0 comments:

Post a Comment