Saturday, June 30, 2012


Mashabiki wa Ujerumani
Wasimamizi wa soka Ujerumani kuwasilisha malalamiko kwa UEFA kufuatia picha za awali za mwanamke akilia katika matangazo ya moja kwa moja

Wasimamizi wakuu wa televisheni nchini Ujerumani wamesema watawasilisha malalamiko yao rasmi kwa wakuu wa soka barani Ulaya, kufuatia picha za shabiki mmoja aliyetokwa na machozi zikionyeshwa, mara tu baada ya Italia kufunga goli la pili katika michuano ya Euro 2012 katika mechi ya nusu fainali dhidi ya Ujerumani.
Shabiki huyo, ambaye ni mwanamke, alikuwa amejipaka rangi zilizomo katika bendera ya Ujerumani, na alielezea kwamba alitokwa na machezo wakati timu ya Ujerumani ilipokuwa ikiingia uwanjani, na wala sio baada ya timu hiyo kufungwa.

Anasema alitokwa na machozi kwa msisimko wa kuwatizama wachezaji wa timu ya nyumbani.
Hii ndio pia Wajerumani wengi waliitizama wakiwa nyumbani.
Wakati Ujerumani ilipoingia katika mashindano hayo, ndio timu iliyotazamiwa na wengi kupata ushindi, na kinyume na hayo, picha walioitizama ya mwanamke kijana akibubujikwa na machozi, na aliyejipaka rangi za bendera ya Ujerumani, nyekundu, manjano na nyeusi, ni jambo ambalo liliwaudhi mashabiki wengi wa Ujerumani.
Suala muhimu hapa ni kwamba mambo hayakuwa hivyo.

Picha hiyo ilitumiwa wakati wa kuonyesha matangazo ya moja kwa moja, na wengi wakadhani mwanamke huyo alikuwa akilia wakati huo.
Hiyo haikuwa mara ya kwanza.
Mapema katika michuano hiyo, kocha wa Ujerumani, Joachim Loew, alionekana akifanya utani na kijana mmoja wa kukimbilia mipira uwanjani, huku akionekana kufurahi, na timu yake ikiendelea kupambana uwanjani, na haikueleweka kwa nini alikuwa akitabasamu na kufurahia hayo.
Picha hiyo ilikuwa imepigwa wakati wa mazoezi, na kisha kutumiwa katika matangazo ya moja kwa moja.
Sasa wanaosimamia matangazo ya televisheni nchini Ujerumani wanasema matangazo ya moja kwa moja lazima yawe hivyo, na pasipo udanganyifu kwa kutumia picha zilizonaswa mapema.

0 comments:

Post a Comment