Thursday, June 28, 2012


 Mwili wa Marehemu Mtoto mchanga ambaye hayafahamika mama yake amekutwa ametupwa karibu na Msikiti wa Soweto Mbeya Asubuhi hii.

 Wakazi wa eneo hilo wakiwa wamefika kushuhudia Kichanga kilicho tupwa eneo la Soweto Mbeya asubuhi hii 

 Picha ya juu na hii ya chini ndivyo zinavyo onekana baada ya mtoto huyo kufumuliwa kutoka kwenye mfuko huo wa salfet unao onekana akiwa amesha fariki, Hiyo nguo ni msamalia mwema ametoa 
 Polisi wamesha fika eneo la Tukio na kuchukua mwili wa mtoto huyo asiye na hatia 
 Polisi akiwa wanaonekana anaondoka na Mwili wa Marehemu eneo la tukio 
 Mbele ni Msikiti wa Poilisi ambao unaonekana na Huku Polisi akiendelea na safari 
 Baadhi ya mashuhuda wakitazama mtoto akiondolewa eneo hilo 

Polisi Ndio wanaondoka eneo la tukio sasa 

**************

Katika hali ya kutatanisha wananchi wa Soweto jijini Mbeya wamekutana na Kifurushi ambacho ndani yake kulikuwa na mtoto mchanga amewekwa na kutupwa akiwa amefariki, ikiwa ni tukio la pili kutokea eneo hilo baada ya tukio kama hilo kutokea wiki mbili zilizopita.
 Hata hivyo akiongea na baadhi ya wananchi ambao hawakupenda kutaja majina yao wamedai kwamba kuna dispensary jirani hapo ambayo hawakutaka sema ni hospital ipi ambapo wana wasi wasi kwamba hutoa Mimba mabinti na kuwatupa eneo hilo.
Mbeya yetu tunafanya uchunguzi wa kina kama ni kweli maelezo ya wadau na tunafuatilia kama kweli Dispensary hiyo ipo.

0 comments:

Post a Comment