Monday, June 25, 2012


Na Mwandishi Wetu 
MAMA wa Wema Isaac
Sepetu, Mariam Sepetu ametoa
kichekesho cha mwaka baada
ya kufanya mahojiano na Tv
moja ya jijini Dar akilenga
kumsafisha mwanaye kwa kuwananga marafiki na
magazeti pendwa, Ijumaa lina
ripoti kamili.
Katika mahojiano hayo, Mama
Wema ‘alibwabwaja’ mengi
huku akitupia lawama makundi mengine wakiwemo
marafiki wa kiume wa
mwanaye. AJISIFU KUMLEA WEMA
VIZURI
Bila soni wala aibu, mzazi
huyo alijisifu kumlea VIZURI
Wema, jambo lililoibua
maswali miongoni mwa watazamaji wa runinga hiyo
huku wengine wakiomba
kamusi ya Kiswahili sanifu ili
kujua maana ya neno ‘vizuri’.
“Japo sikumnyonyesha lakini
mwanangu nimemlea vizuri. Ana maadili mazuri ya
Kiafrika,” alisema mama huyo. AFUNGUKA BILA BREKI
Katika mahojiano hayo
aliyoyafanya Juni 19, mwaka
huu, mama huyo aliwashushia
lawama mashoga wa
mwanaye akisema walimpoteza Wema kwa
kumpeleka kwa waganga wa
kienyeji kipindi cha nyuma na
kumfanya awe
‘mawengemawenge’.
“Nimehangaika sana usiku na mchana kumfanya
mwanangu arudi kwenye hali
yake ya kawaida. Marafiki
zake walimpoteza,
walimpeleka kwa waganga
kitendo ambacho kilichangia kwa kiasi kikubwa
kumpoteza mwanangu,
akawa mtu asiyejielewa,”
alifunguka bila breki. ALIKOROGA, ATALINYWA
Kwa kauli hizo tu, Ijumaa
lilipokea simu nyingi kutoka
kwa mastaa na wasomaji wa
kawaida wakidai kuwa
mama huyo alikuwa amewachekesha kwani tangu
kipindi hicho kilipokwenda
hewani siku hiyo, marafiki
wote wa Wema waliamua
kujichenga na kumwachia
maisha ya peke yake huku wakidai kama anataka kuishi
kwa raha atafute kisiwa cha
kuishi huko.
“Mdomo uliponza kichwa, sisi
ni marafiki zake na tunafanya
naye kazi kwa upendo mkubwa lakini kwa kauli ya
mama tunaonekana
tunajipendekeza. Acha aishi
dunia ya peke yake,” alisema
mmoja wa waigizaji kiwango
hapa Bongo. TURUDI KWA MAMA WEMA
Akiendelea kuropoka mambo
bila kuanika ushahidi wa
wazi, mama huyo alisema
marafiki wote wa Wema ni
wanafiki na kama mwanaye anataka marafiki wa kweli, ni
yeye mama, dada yake Wema
(pengine yule anayeishi
Kumekucha- Sinza) na ndugu
wengine wa karibu. ETI WEMA MAMBO SAFI
Mama Wema alifunguka
kuwa katika kipindi hiki
ambacho mwanaye mambo
yake yanamwendea vizuri
hataki marafiki wanafiki wanaomfuatafuata Wema
kwa lengo la kumchafua. SNURA ACHAFUKA
Awali kabla mama Wema
hajaanza kutiririka runingani,
msanii wa filamu Snura Mushi
aliongea akisema yeye na
Wema ni marafiki wakubwa mpaka watu wanamsema
vibaya kwamba, amekuwa
mpambe wa Miss Tanzania
huyo wa mwaka 2006.
Snura akasema wao
wanapendana sana, watakuwa sambamba hadi
siku kila mmoja atakapoishi
maisha mengine. Wema naye
alikazia hapo kwa kukiri
yeye na Snura ni marafiki
wakubwa. Lakini mama Wema
alipopewa muda wa kuwa
hewani, alimchana hadi Snura
kwamba ni walewale. Hebu
msikie:
“Mwanangu Wema, nakwambia mimi mama
yako, jihadhari na marafiki
wanafiki. Rafiki wa kweli ni
yule anayekujali, wengine
wanafiki. Haohao ndiyo
wanaokucheka ukiandikwa vibaya kwenye magazeti,
wewe huna rafiki wa kweli.” HIVI ALIJIULIZA HILI SWALI?
Kwa mujibu wa wadau
wengi waliopiga simu
kwenye dawati la Ijumaa
walihoji kwa nini mzazi huyo
hakuanika chanzo cha utajiri wa Wema na kumhoji
mwanaye alikopata Sh.
milioni 400 za kununulia
nyumba (ingawa imebainika
si yake) kwani hana filamu
aliyocheza ikamwingizia mkwanja huo wote. WOLPER NAYE HAKUWA
SALAMA
Katika tuhuma hizo, mama
Wema alimshambulia
mwigizaji Jacqueline Wolper
akidai alimkosea mwanaye (kipindi hicho alichopotea)
kwa kumwambia kuwa
amchezeshe filamu moja ili
amlipe fedha ya kwenda
kununua kitanda wakati
yeye anaamini mwanaye kamwe hajawahi kukumbana
na tatizo la kukosa mahali pa
kulala katika maisha yake. KITUKO
Wakati akihojiwa, mama
huyo alionesha kitanda
kipyaaa na cha kisasa akidai
ndicho alichokuwa akilalia
Wema tangu akiwa mdogo hadi leo ana miaka 23. Hata
hivyo, kitanda hicho
kilionekana kama
kimenunuliwa jana yake.
WOLPER ASHINDWA
KUJIZUIA, AMJIBU MAMA WEMA
“Mh! Sijui ataelewekaje huyo
mama na tena kwa bahati
mbaya huwa sitazami hizo
local channel (televisheni
inayotazamwa na eneo fulani pekee) ambazo nasikia ndiyo
ametumia kunizungumzia na
kunishirikisha mimi na
mwanaye. Mimi huwa
natazama DSTV. Niliambiwa na
watu walioona.” AORODHESHA WANAUME WA
WEMA
Akitambaa na msururu wa
wanaume waliotoka
kimapenzi na mwanaye (bila
kujali kuwa siyo maadili kwa binti wa Kiafrika), mama
Wema alisema ni kweli
mwanaye ‘amesharukaruka’
na vijana wawili watatu.
Aliwataja marehemu Steven
Kanumba (alithibitisha alijua) kuwa alikuwa miongoni
mwa wanaume wa Wema
huku akimshukuru na
kumuomba Mungu amrehemu
huko mbele za haki aliko.
Pia mzazi huyo alimtaja mjasiriamali, Jumbe Yusuf
Jumbe na kumalizia na
mwanamuziki mkali wa
Bongo Fleva, Nasibu Abdu
Juma ‘Diamond’ kuwa hao
ndiyo wanaume wa Wema pekee.
Majina hayo siyo mageni
kwani ni yaleyale
yaliyokuwa yakichorwa na
magazeti pendwa ingawa
alimsahau mwanamuziki wa Mashujaa Band, Charles Gabriel
‘Chaz Baba’ huku Wema
mwenyewe akiomba majina
ya wasanii Khaleed Mohamed
‘TID’ na Herry Samir ‘Mr Blue’
yakatwe kwenye listi. MTITI KWA DIAMOND
Mariam alipofika kwenye jina
la Diamond, ndipo akawaka si
kitoto akidai kuwa hakuwahi
kumtarajia kama anaweza
kuwa mkwewe hata siku moja kwani ni mpuuzi na
mhuni.
“Mtu wamekutana tu huko,
bila kushirikisha wazazi
anamvalisha pete kwenye
klabu za muziki. Nilishajua mwisho wake sababu ni
mhunimhuni tu aliyemtumia
mwanangu kama daraja la
kupandia afike anakotaka.” LAKINI TUJIKUMBUSHE
Wakati Wema anamtongoza
Diamond kupitia mtandao wa
kijamii wa Facebook mwaka
2010, tayari ‘kichaa’ huyo wa
Bongo Fleva alikuwa juu kwani tayari alishavunja
rekodi kimuziki kwa kutwaa
tuzo tatu za Kili hivyo si
kweli kwamba alitaka
umaarufu. FAMILIA YA DIAMOND
Kwa mujibu wa chanzo
kilicho karibu na familia ya
Diamond kilipenyeza habari
kuwa, hawakufurahiswa na
kitendo cha mama Wema kulipuka runingani kwani
hata mama Diamond naye ana
uwezo wa kufanya hivyo. WEMA VIPI?
Baada ya kipindi hicho
kwenda hewani, Wema
aliwasiliana na chumba chetu
cha habari akilia na kuhaha
kuwa mama yake alikuwa amezungumza vitu ambavyo
hata yeye hakutarajia (meseji
zake tunazo). ONYO LA MAGAZETI PENDWA
Katika kipindi hicho, mama
Wema alipigilia msumari wa
mwisho pale alipoyapa mwezi
mmoja magazeti pendwa
yaache kumwandika mwanaye.
“Haya magazeti ya udaku
(pendwa) nayapa mwezi
mmoja kuanzia leo hii
ninavyoongea, yaache
kumwandika mwanangu, safari hii wajue hawadili na
Wema, wanadili na mimi
mama yake.
“Wewe Shakoor wewe,
Shakoor (Jongo). Si
unajifanya upo karibu sana na Wema kumbe mnafiki
mkubwa, nilishawahi

kukupopoa mawe, hujakoma,

0 comments:

Post a Comment