Monday, June 11, 2012


Mapigano Syria
Kiongozi mpya wa baraza la kitaifa la upinzani nchini Syria, (SNC) ametoa wito kwa maafisa wa serikali ya rais Bashar Al Asaad, mjini Damascus, kuanza kuondoka serikalini.

Akiongea mjini Istanbul, Uturuki, Abdelbaset Sayda alipinga kwa mara nyingine hatua ya jamii ya kimataifa kuingilia mzozo wa Syria hadi pale Umoja wa mataifa utakapoamrisha.
Wakati huohuo, vurugu limekithiri mjini Homs, huku milipuko ikisikika pamoja na milio ya risasi mapema leo.
Takriban watu 35 waliuawa katika mapigano mengine mabaya mnamo siku ya Jumapili, kwa mujibu wa wanaharakati.

Kulingana na taarifa ya mwandishi wa BBC Paul Danahar, aliye mjini Homs, licha ya mapigano kuna shughuli nyingi tu mjini humo ingawa sehemu ya mji huo ambako mapigano yamekuwa yakiendelea imefungwa.
Abdelbaset Sayda, alifahamisha BBC kuwa baraza hilo halitaki jamii ya kimataifa kuingilia mzozo wa Syria. Lakini utawala wa Asaada ndio utalazimisha hilo kufanyika. Hatua hiyo amesema ni kusababisha vita visivyohitajika kwa taifa na watu kwa ujumla.

"Nia yetu ni kutumia njia salama kusuluhisha mzozo, lakini huu utawala wa kinyama unafanya mauaji na kutumia kila mbinu kuafikia malengo yao" alisema Abdelbaset.
Bwana Sayda, anayeishi uhamishoni nchini Sweden, alisema kuwa hali nchini Syria sasa inaingia katika awamu yake muhimu na kwamba utawala wa rais Bashar al-Assad umeanza kulemewa.

"Mauaji yanayofanyika pamoja na ongezeko la mashambulizi ya makombora ni ishara kuwa serikali inakabiliwa na wakati mgumu" alisema bwana Assad.
Pia aliwashawishi maafisa wa serikali ya Asaad kuanza kuondoka serikalini.
Mwandishi wa BBC mjini Beirut, Jim Muir, anasema kuwa baadhi ya maafisa wamekuwa wakiondoka serikalini ingawa wachache sana.

0 comments:

Post a Comment