Wednesday, June 27, 2012

Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamanda Suleiman Kova, akizungumza na waandishi wa habari leo mchana kuhusu tukio la utekaji nyara na kujeruhiwa kwa kiongozi wa mgomo wa Madaktari,  Steven Ulimboka, anayedaiwa kutekwa na watu watano wakati akipata kinwaji katika klabu ya Leaders Kiondoni jijini Dar es salaam.

Kamanda Kova amesema Ulimboka aliokotwa na msamaria mwema ambaye hakutaka kumtaja jina lake kiusalama na kutoharibu upelelezi na kuwa msamaria mwema huyo alimuokota Ulimboka katika msitu wa Mabwepande na kutoa taarifa kituo cha polisi cha Bunju, ambapo polisi aliyekuwa zamu alichukua maelezo yake na baadae, Steven Ulimboka, kuletwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.

Kamanda Kova amesema jeshi la Polisi Kanda Maalum, limeunda jopo maalum kwa ajili ya uchunguzi na upelelezi wa tukio hilo la utekaji nyara, kwani ni tukio la kwanza kutoke nchini, ameongeza kwamba wahusika wote watakaobainika kuhusika na tukio hilo watachukuliwa hatua za kisheria na sheria itafuata mkondo wake ili kukomesha matukio mengine kama hayo.
Waandishi wa habari wakimsikilza kamanda Suleiman Kova katika kituo kikuu cha Polisi Kati jijini Dar es salaam, leo mchana.

0 comments:

Post a Comment