Sunday, June 10, 2012

 
Waziri wa mambo ya ndani Prof. GEORGE SAITOT na naibu wake JOSHUA OJODE wamefariki dunia leo kwa ajali ya HELICOPTER
 Kutoka BBC Swahili:
Waziri wa Usalama wa ndani Profesa George Saitoti na Naibu wake Orwa Ojode wamefariki dunia katika ajali ya helikopta ya polisi iliyotokea leo asubuhi katika eneo la Kibiku, karibu na mji wa Ngong takriban kilometa ishirini kutoka mji mkuu wa Nairobi.
Abiria wote saba waliokuwa kwenye helikopta hiyo wamefariki dunia na miiliyao kuteketezwa kwa kiasi cha kutoweza kutambulika.
Kilichosababish

a ajali hiyo bado hakijabainika.
Bwana Saitoti na maafisa wengine wa juu katika wizara ya usalama wa ndani walikuwa wakielekea katika eneo la Sotik kwa mkutano wa usalama. Saitoti alikuwa miongoni mwa wanasiasa mashuhuri nchini Kenya waliokuwa wakipania kugombea kiti cha urais katika uchaguzi mkuu ujao.
Walioshuhudia ajali hiyo wamesema waliona helikota hiyo ikizunguka angani kabla ya kuanguka katika msitu wa Ngong.
Polisi wamezingira eneo la ajali hiyo nakamishna wa polisi Mathew Iteere aliyepo katika eneo la ajali anatarajiwa kutoa taarifa kamili kuhusiana na ajali hiyo.
Ajali hiyo ya helikopta imetokea katika siku ambapo Kenya inaadhimisha miaka minne tangu kutokea ajali ya ndege iliyowauwa mawaziri wengine wa serikali, Kipkalya Kones na Lorna Laboso

0 comments:

Post a Comment