Wednesday, May 9, 2012

Matatizo Ukraine
Matatizo Ukraine
Mashindano ya Fainali ya Kombe la soka kwa Mataifa ya Ulaya, Euro 2012 yanayoanza mwezi juni mwaka huu yalikua nuru mpya kwa taifa la Ukraine kushamiri kwenye medani ya kimataifa na pia kuimarisha uchumi wake unaolegalega.
Badala yake iliyokua fursa ya kujikwamua matatizo limekua tatizo.
Katika hatua inayofananishwa na vita baridi, wakuu wa ngazi ya juu kutoka Muungano wa Ulaya wameapa kua watasusia mechi zote zitakazopangwa Ukraine kwa sababu ya madai kuhusu kunyanyaswa kwa Waziri Mkuu wa zamani Yulia Tymoshenko gerezani.
Wakosoaji wameonya kua mashabiki wa soka huenda wakashindwa kuhudhuria mechi kutokana na viwango vikubwa vya bei za kulala hotelini na kwamba serikali ambayo ina upungufu wa fedha imeiweka nchi hio katika hali mbovu ya uchumi kwa kutumia dola bilioni 14 kuandaa mashindano haya.
Hi ilikua fursa kwa nchi hii kujiuza na kuonyesha kiwango chake kwa sababu ya wandishi wa habari watakaokwenda huko kwa ajili ya mashindano, amesema Oleh Rybachuk, hapo zamani Waziri katika serikali ya kwanza ya Bi Tymoshenko.
Bw.Oleh ameongezea kusema kua, hivi sasa, wandishi watakuja kuandika juu ya matatizo mengi kupita kiasi.
Nchi ya Ukrainer ilipewa nafasi ya kuandaa mashindano ya Euro 2012 kwa ushirikiano na Poland mnamo mwaka 2007 katika hatua iliyobainika kama zawadi kwa nchi hizi mbili hapo zamani za Kikomunisti zinazopenda soka.
Wafuasi wa Tymoshenko
Wafuasi wa Tymoshenko
Wakati huo uchumi wa Ukraine ulikua mzuri na nchi za magharibi zilifurahia juhudi zake za kukumbatia sera ya demokrasi kufuatia maandamano makubwa ya mwaka 2004 yaliyojulikana kama ''Orange Revolution'' yaliyochagiza kuundwa kwa serikali inayopendelewa na Mataifa ya magharibi.
Ukraine ya leo ni tofauti na ya wakati huo.
Shujaa wa mageuzi yaliyosababishwa na vuguvugu la Orange, Tymoshenko, wakati huo akiwa kiongozi wa upinzani, anatumikia kifungo cha miaka saba kwa kutumia vibaya madaraka.
Nchi za magharibi zililalamikia kifungo chake mwaka jana na kudai kua ni kisingizio cha siasa kilichopangwa na utawala wa Rais Viktor Yanukovych, ambaye ushindi wake wa mwaka 2004 uliogubikwa na tuhuma za kuibia kura ulingatuliwa na Bi.Tymoshenko.
Tymoshenko, mwenye umri wa miaka 51, kwa zaidi ya wiki mbili amesusia chakula baada ya habari kwamba walinzi wa jela walimfunga ndani ya shuka na kumpiga ngumi za tumbo, huku akilia na kupiga kelele za kutaka asaidiwe.
Tangu hapo alikua na maumivu makali ya mgongo.
Picha za majeraha makubwa ya tumbo la Bi.Tymoshenko na kwenye miguu zilizotolewa na shirika maarufu nchini humo la haki za binadamu, zimeushangaza ulimwengu na kua sababu ya Maofisa wa Muungano wa Ulaya, akiwemo Rais wa Muungano Herman Van Rompuy, vilevile Rais wa tume ya Ulaya Jose Manuel Barroso, halikadhalika serikali za Austria na Ubeligiji zimesimamisha mipango ya kuhudhuria mechi zitakazochezwa huko Ukraine.
Chancellor Angela Merkel wa Ujerumani amedokeza kua ataweza kuzuru nchi hio wakati wa amshindano ikiwa serikali itabadili jinsi inavyomtunza Bi.Tymoshenko.
Katika tukio la aibu zaidi kwa nchi hio, imebidi mipango ya kikao juu ya ushirikiano wa Mataifa ya Ulaya ya kati na mashariki kwa sababu viongozi wengi walisusia kutokana na suala la kuteswa kwa Tymoshenko.
Ikiwa hayo hayatoshi kuichafulia jina Ukraine, Mkuu wa UEFA, Michel Platini amelalamika juu ya viwango vya bei ya hoteli na kuitaka serikali isiwaruhusu majambazi kuwapora wapenzi wa soka.
Katika vichekesho vingine, tangazo la TV huko Uholanzi limezua kasheshe kuhusu mashindano ya EURO 2012.
Kampuni ya umeme ya Uholanzi katika tangazo la biashara lililotolewa hivi karibuni inawashauri wanawake wasiwaruhusu waume wao kuhudhuria mechi za Ukraine kwa sababu hawawezi kuponyoka urembo wa wanawake wa Ukraine. Ukraine imelalamika na kusema tangazo hilo ni la kiubaguzi.

0 comments:

Post a Comment