Wednesday, May 9, 2012

                                                Mwalimu Ayoub Mangi
Miongoni mwa adha kubwa zinazowakabili wakazi wa Dar ni msongamano mkubwa wa magari, hupoteza muda mwingi ambao madhara yake kiuchumi ni makubwa sana. Mafuta yanatumika mengi na muda wa uzalishaji kuwa mdogo.
Timu ya Bahari ya maarifa ailiongea na Mwalimu Ayoub Mangi,alibainisha mambo kadhaa kwa kusema " Msongamano huu mkubwa husababishwa na ubinafsi wa watu na miundo mbinu kuwa duni, familia moja inaingiza magari matano yakiwa na mtu mmoja mmoja tu kwanini msongamano usitokee? miundo mbinu haindani na wakati. Ili tuondokane na msongamano tunatakiwa kuhakikisha gharama za usafiri wa umma zinakuwa chini sana ili watu wengi watumie usafiri wa umma, ukiwa kwenye msongamano utaona magari mengi yana mtu mmoja mmoja yapo kwenye msongamano hasa mida ya kutoka kazini na kwenda kazini."
  Aliendelea kuchambua " Sehemu za vivuko nazo zinatakiwa kuwa za chini ya ardhi ( Underground ) mfano Manzese pale darajani siku hizi hamna msongamano, magari yaendayo kasi pia ni chachu nzuri ya kumaliza tatizo, treni za umeme hazikwepeki. Serikali ipunguze kodi magari ya abiria na iongeze kodi kubwa kwenye magari haya ya binafsi, pia ihimize uingizaji wa magari mapya. Pia misafara ya viongozi ilipie kodi, kwa uzoefu wangu kukaa Dar nimebaini mwezi desemba msongamano hupungua kabisa na saa zingine huisha ila unahamia barabara za Moshi" ndivyo alivyonena Mwalimu Ayoub.
   Kama wengine wanazo kero za kukosa usafiri Dar ni magari mengi tena mengine yamefungiwa majumbani.

0 comments:

Post a Comment