Monday, May 14, 2012

Mabingwa wa mpira wa Miguu Tanzania Simba ya Dar es salaam, usiku wa tarehe 13 May 2012 imeyaaga mashindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kufungwa magoli 3 - 0 na Al-Ahly Shandy ya Sudan kwenye muda wa kawaida. 
  
Magoli yote hayo yalifungwa katika kipindi cha pili, la kwanza likiwa dakika ya kwanza kipindi cha pili, yakifuatiwa na jingine dakika 3 baadaye. La tatu lilifungwa baada ya dakika 10 baada ya goli la pili kwa uzembe wa Victor Costa kwa kutokuwa makini na utoaji wa pasi na hivyo kupoteza mpira huo uliomfikia mchezaji wa Al-Ahly Shandy aliyefunga kwa urahisi. Mwisho wa dakika 90 mabao yalikuwa 3 - 0 dhidi ya Simba, na hivyo kufanya kuwe na jumla ya mabao 3 - 3.  
     
Mshindi alipatikana kwa njia ya penati ambapo jumla ya penati 10 zilipigwa. Juma Kaseja alishindwa kufunga penati ya mwisho kwa Simba na hivyo kuzidiwa bao moja na Al-Ahly Shandy 
  
Simba wanatarajiwa kurudi Dar es Salaam Jumatatu, ili waanze kuganga mashindano mengine.

0 comments:

Post a Comment