Wednesday, May 9, 2012

Msanii nguli wa vichekesho na Maigizo anayejulikana zaidi kama King Majuto, leo mchana ameongea na Bongo5 na kuthibitisha kuwa amekula bingo ya kuwa mmoja kati ya Brand Ambassadors wa Kampuni ya Azam kwa kitita kinono.

Mzee Majuto amesema ameingia mkataba wa miaka miwili ya kufanya matangazo yote ya bidhaa za Azam.
Alipoulizwa kuhusu mkataba wake na Rihamma, Mzee Majuto amesema, ‘Mimi nimemlipa fidia baada ya kukubaliana naye malipo ya kuvunja mkataba ambayo imefikia kiasi cha shilingi za kitanzania milioni 20.’
Big Up Mzee Majuto

0 comments:

Post a Comment