Thursday, May 10, 2012

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya picha ya ramani ya Tanzania, kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Ramani Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Vincent Mugaya, baada ya kufunga awamu ya kwanza ya maandalizi ya sensa ya watu na makazi iliyofanyika leo Mei 9, 2012, Mkoani Tabora.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia wananchi wa mkoani Tabora wakati akifunga awamu ya kwanza ya maandalizi ya sensa ya watu na makazi iliyofanyika leo Mei 9, 2012 katika Uwanja wa Chipukizi mkoani Tabora.
 Makamu akiwasili kwenye uwanja wa chipukizi mkoani Tabora kufunga awamu ya kwanza ya maandalizi ya  sensa ya watu na makazi iliyofanyika leo Mei 9, 2012 katika Uwanja wa Chipukizi mkoani Tabora.

Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi Ya Makamu Wa Rais

0 comments:

Post a Comment