Wednesday, May 16, 2012



Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Haruni Sanchawa na Makongoro Oging'
MAISHA ya msanii maarufu ya filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ambaye yupo katika Gereza la Segerea, yamebainika baada ya gazeti hili kunasa ukweli jinsi anavyoishi gerezani humo.
Lulu ambaye anadaiwa kuhusika na kifo cha aliyekuwa msanii maarufu wa filamu, Steven Kanumba ‘The Great’ kilichotokea Aprili 7, mwaka huu, imeelezwa kuwa maisha yake ya mahabusu yanasikitisha.
Vyanzo vyetu kutoka katika Gereza la Segerea vinasema msanii huyo licha ya kuwa analetewa chakula kutoka nyumbani kila siku, huwa anakula baada ya kubembelezwa na baadhi ya mahabusu wenzake.
“Lulu siyo yule mnayemfahamu uraiani, humu gerezani amekuwa mtu wa kusikia kile anachoambiwa na wenzake, amekuwa msikivu sana na hupenda kulala mara kwa mara,” kilisema chanzo hicho.
Habari zinasema msanii huyo amekuwa akifundishwa aya kwa aya za Biblia na amekuwa mwepesi kushika baadhi ya mistari ya kwenye kitabu hicho kitakatifu kwa Wakristo.
“Bila shaka amekuwa akishika aya kwa kuwa alizoea kushika maneno yaliyokuwa yanaandikwa katika script za michezo ya filamu,” alisema askari mmoja wa magereza aliyeomba jina lake kutoandikwa gazetini.
Alisema kinachosikitisha ni pale anapotembelewa na rafiki zake kwani wakiondoka Lulu hushinda akilia mchana kutwa.
Aliongeza kuwa hali anayoishi nayo msanii huyo gerezani ni ya kutia huzuni na simanzi na haonekani kuzoea mazingira kama walivyo mahabusu wengine.
Hivi karibuni, ilielezwa kuwa Lulu amekuwa akivaa rosari na kusoma Biblia mara kwa mara kutokana na mafunzo anayopewa na baadhi ya walokole waliofungwa katika gereza hilo.
CHANZO CHA HABARI HII NI GROBAL PUBLISHERS.INFO

0 comments:

Post a Comment