Tuesday, May 29, 2012

Jaji Mkuu nchini Ufilipino anasimamishwa wathifa huo baada ya kushindwa kutangaza mali zake ambazo ni za mamilioni ya dola. Baada ya kufika mbele ya baraza la Senate, Jaji Mkuu, Renato Corona, alipatikana na hatia ya kuhujumu imani ya raia ambayo ni kinyume na katiba ya nchi.

Pia afisa huyo ametuhumiwa kwa kumlinda Rais wa zamani, Gloria Arroyo, ambaye kwa sasa yuko kizuizi cha nyumbani kwa makosa ya wizi wa kura na ufisadi.
Hatua ya sasa imeonekana kama ushindi mkubwa kwa Rais Benigno Aquino, aliyeahidi kukabiliana na ufisadi kama hatua ya kuboresha uwongozi nchini Ufilipino.

CHANZO BBC SWAHILI

0 comments:

Post a Comment