Wednesday, May 16, 2012



Mbunge wa Iringa(Chadema) Akiongea na wafuasi wa chadema baada ya kesi kuhairishwa mpaka tarehe 30/5/2012 itakapotajwa tena

Wananchi Wakisubiri Kusikiliza Kesi Mahakamani Mapema leo
Mtuhumiwa Wa kutishia Mauaji Diwani wa CCM kata ya Nduli Idd Chonanga akiwasili mahakamani tayari kwa kusomewa mashitaka yanayomkabili
Mbunge wa iringa Mjini Mch Peter Msigwa(Chadema) akifuatilia Kesi ndani chumba cha mahakama ya mkoa Iringa
(Picha zote na Said Ng'amilo wa Mjengwa Blog -Iringa)
Kutoka mahakamani
 Hakimu mkazi wa mahakama ya mkoa wa iringa Bi Consolata Singano akiendesha kesi huku akiongozwa na msoma mashtaka wa serikari Ndg msuya, alisema kuwa Mshatakiwa anashitakiwa kwa makosa mawili, moja likiwa ni mnamo tarehe 14/5/2012 katika ofisi za manispaa ya iringa alimtishia kwa maneno Kumuua Mbunge wa Iringa mjini mch Peter Msigwa, shitaka la Pili, tarehe hiyo hiyo alimtishia kumuua diwani wa kata ya mivinjeni(Chadema) Ndg Fredrick Nyalusi, Mshitakiwa alikana shitaka, hakimu alisema dhamana ipo wazi kwa mshitakiwa, lakini wadhamini wa mshitakiwa hawakutimiza masharti ya dhamana hivyo amepelekwa rumande.

Mjengwa Blog itawajuza kinachoendelea  ...

Mbunge Msigwa naye asema haya
Mbunge wa iringa Mch Peter msigwa amewataka wananchi  wa iringa kuwuawatulivu  katika kipindi cha vurugu za kisiasa, wasiwe chanzo cha  fujo na machafuko ya aina yoyote na waendelee na shughuli za ujenzi wa taifa kama kawaidaingawa ameshangaa mpaka sasa hakuna kiongozi wa serikari ya mkoa aliyekemea kitendo hicho kisichokuwa cha kiungwana

0 comments:

Post a Comment