Thursday, May 10, 2012

Basi la kampuni ya Muro Investment, lenye namba za usajili T820BEY lillilokuwa likitokea Mwanza kwenda jijini Dar es Salaam, limewaka moto na kuteketea  kabisa maeneo ya Maseyu, Mkoani Morogoro. Ajali hiyo iliyotokea majira ya saa 1:15 usiku  wa Mei 8, 2012, haikusababisha madhara kwa abiria isipokuwa mali zao zote ziliteketea kwa moto
 Magari yakipita pembeni ya basi hilo lililokuwa likiteketea kwa moto na hapakuwa na askari wala magari ya zima moto yaliyoweza kuwahi kufika na kuzima moto huo ulioliteketeza basi hilo kabisa.
 Basi hilo likizidi kuteketea kwa moto.
Wakazi wa Maseyu na wasafiri wakiangalia basi hilo likiteketea kwa moto.
Kwa mujibu wa mmoja wa wahusika wa basi hilo ni kwamba chanzo cha ajali ilikuwa hitilafu ya umeme iliyotokea katika gari hilo. Inadaiwa kuwa gari hilo lilipata hitilafu katika taa na walipofika mjini Morogoro walifanyia marekebisho na kuendelea na safari na walipofika maeneo hayo ya Maseyu likashika moto.

0 comments:

Post a Comment